Kwenye Mahojiano katika MWC 2022, Mtendaji mkuu wa samsung alisema kua ingawa hakutakua na muendelezo wa matoleo ya Note kwa siku zijazo, hivyo baadhi ya vitu ambavyo vilikua vya kipekee kwenye simu hiyo vitawekwa kwenye matoleo mengine ya brand hiyo mfano uwepo wa ultra zote kwenye Gallaxy S.
uchambuzi wa juu ya mabadiliko haya kutoka katika maoni ya Dailian ( ambayo yalitafsiriwa na (9to5Google) Mkuu wa uzoefu wa simu ya mkononi wa Samsung, Roh Tae-Moon alisema "Galaxy Note itatoka kama Ultra kwenye matoleo mengine" Taarifa ni fupi lakini ni wazi kua hakutakua na simu za matoleo ya Note tena kwenye kampuni ya simu za mkononi za Samsung, lakini bado unaweza kuendelea kupata vitu vyao vyote haswa kwenye vipengele uvipendavyo ndani ya samsung Ultra ambazo zinatolewa kwa matoleo ya S.
Utafiti mdogo ambao tumeufanya sisi kama ZOOM Tech ili kuhakikisha ukiacha na taarifa zinazoendelea ila pia kutoa yamkini kwa taswira za Watanzania na hivyo tumeona tukupe mifano michache kuhusu taarifa hii, Kwa toleo la S kutoka samsung hapa tunaiweka dhahiri Samsung S22 simu hii inakuja na Peni ambayo inatumika kama kimonyezeo kwenye simu yako na ni peni ambayo zilikua kwenye matoleo ya note tuu hapo awali, ila pia s22 inakuja na vipengele vingi mfano vya UI ambavyo vilianzishwa rasmi na samsung Note. hii ni baadhi ya mifano sio kwamba kampuni hii inaua tuu toleo hili ila ina kuwekea kwenye toleo lao lingine ambalo ni Samsung S, na kwa matoleo mengine yote ya samsung S utakutanana na vipengele vya Note.
Hivyo kwa mtumiaji wa samsung na unatamani kupata vitu vi wili kwa pamoja muda ni wako sasa ndani ya samsung S22 unakutana na vipengele vyote uvipendavyo vya Note na hivyo simu hizi za S22 ultra ni mbadala wa Samsung Note .
Fuatilia makala hizi kila saiku ili kupana nafasi wakuwa wakwanza kufikiwa na kila ujumbe mpya kwenye ulimwengu wa Teknolojia.
#TechLazima
إرسال تعليق