Infinix Note 30 Pro, ni simu ya hali
ya kisasa na bora iliyozinduliwa hivi karibuni na kampuni ya Infinix, simu hii
inakuja na sifa bora ambazo ni pamoja na Teknolojia ya Fast Charge Watt 68,
Wireless Fast Charge Watt 15, kioo cha AMOLED, kamera yenye nguvu ya 108MP,
uhifadhi mkubwa pamoja na battery yenye kudumu na chaji kwa muda mrefu.
Kupitia makala hii tutaenda tutapata
kuifahamu Infinix NOTE 30 Pro kiundani zaidi.
Fast
Chaji yenye Spidi
Simu hii ina betri ya Li-Po yenye
uwezo wa 5000 mAh, ambayo inafanya simu yako kudumu na chaji siku nzima bila kuchaji.
Pia kama unahitaji kuchaji simu yako kwa uharaka, Infinix Note 30 Pro inakuja
na teknolojia ya fast charging ya hadi 68W, ambayo inaweza kuchaji betri ya
simu hiyo hadi asilimia 80 ndani ya dakika 30 tu.
Pia, Infinix Note 30 Pro inakuja na
teknolojia ya wireless charging ya 15W ambayo pia inaweza kufanya simu hiyo
kuchaji simu nyingine kwa kutumia wireless.
Kioo
cha AMOLED
Infinix Note 30 Pro inakuja na kioo
cha AMOLED chenye ukubwa wa inchi 6.78. Kioo hiki kinaonyesha rangi zenye kina,
huku kikiwa na uwezo wa kuonyesha rangi zaidi bilioni 1 kupitia resolution ya
1080 kwa 2460 pixel. Utaweza kungalia video na picha kwenye mitandao ya kijamii
kwa upana kwani kioo hichi ni kipana na kisichokuwa na kingo kubwa yaani Full
Display.
Kamera
yenye Nguvu
Moja kati ya sifa kubwa ya Infinix
Note 30 Pro ni mfumo wake wa kamera ambapo inakuja na kamera tatu za nyuma huku
kamera kuu ikiwa na Megapixel 108MP huku ikisaidiwa na kamera ya pili ya 2MP,
na kamera ya tatu ya QVGA.
Hii inamaanisha kuwa unaweza kupiga
picha zenye muonekano mzuri na zenye details zaidi hasa kama wewe ni mtumiaji
wa mitandao ya kijamii, mtumiaji wa kawaida au hata kama wewe ni mfanyabiashara
wa mtandaoni.
Kamera hizi zinakuja na flash ya
Quad-LED, HDR, pamoja na panorama, na pia zinaweza kurekodi video za hadi
1440p@30fps au 1080p@30fps. Kwa upande wa selfie Infinix Note 30 Pro ina kamera
ya mbele ya 16MP na flash ya LED, hii itakusaidia kuhakikisha kupata picha bora
hata katika mwangaza hafifu.
Utendaji
Imara
Infinix Note 30 Pro inatumia chipset
ya Mediatek MT8781 Helio G99 (6nm), pamoja na CPU ya Octa-core yenye kasi ya
2.2 GHz Cortex-A76 na 2.0 GHz Cortex-A55. Hii inamaanisha kuwa simu hii ina
nguvu ya kutosha kufanya mambo mbalimbali kama vile kwa wapenzi wa game, na
kazi nyingine kama kuedit video, picha na kutumia programu nyingine bora.
Kupitia GPU ya Mali-G57 MC2 inaboresha uwezo wa kucheza Game na inahakikisha
picha, na video zinaonekana kwa urahisi na kwa ubora mzuri.
Uhifadhi
Mpana
Infinix Note 30 Pro inakuja na
machaguo ya uhifadhi wa ndani wa GB 128 au GB 256. Hii inamaanisha kuwa utakuwa
na nafasi ya kutosha kwa faili zako zote, kama picha, video, na programu
mbalimbali. Mbali na hayo pia kama haitoshi utaweza kuongeza uhifadhi wa ndani
kwa kutumia Memory Card yenye uwezo wa hadi GB 512..
Muundo
wa Kuvutia
Infinix Note 30 Pro inakuja muundo
mzuri na rangi za kuvutia za Magic Black na Variable Gold, ambazo zinafanya
simu hii iwe na muonekano bora na wa kuvutia. Mbali na hayo simu hii pia ina
sensori ya alama ya vidole kwa upande, ambayo ina kuhakikishia usalama kwenye
kifaa chako.
Pamoja na hayo Infinix Kuungana na TIKTOK haijawaacha nyuma watumiaji wake na kuendelea kugawa zawadi kila kona. Msimu huu nikwaajili ya kila mtu kama wewe ni mtumiaji wa TIKTOK unanafasi ya kushinda simu INFINIX NOTE 30 mpyaa kwa kutumia App hii chakufanya record video yako ukiwa unanyesha kipajichako kwa kutumia filter ya infinix (TakechargewithNote30) na record kabla alama ya chaji haijajaa onyesha ubunifu wako huku ukitumia #TakechargewithNote30 na watag @InfinixmobileTz na ujishindie Simu yako mpyaa kabisa.
Hitimisho
Kwa ujumla, Infinix Note 30 Pro ni simu ya kuvutia na yenye sifa bora zaidi. Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanatafuta simu bora kwaajili ya matumizi ya kuchukua picha na video bora kwaajili ya mitandao ya kijamii, au kwaajili kupiga picha bora kwaajili ya biashara yako basi simu hii ni chagua bora sana. Pia kwa wapenzi wa Game pamoja na kutumia Apps mbalimbali simu hii pia inakuja na uwezo mkubwa sana kwaajili ya matumizi hayo.
Pia Kumbuka kuwa #Gusanishaijae ndio hashtag ya kutumia kwani simu hii inakuja na teknolojia ya kuchaji simu nyingine kwa kutumia mfumo wa Wireless. Yaani unaweza kuchaji simu nyingine kwa kuweka simu yako juu ya Infinix Note 30 Pro.
Wasiliana nao 0745170222 wakupe maujanja zaidi.
Вауууу, телефон Infinix Note 30 Pro - самое лучшее что я видел ,а больше всего понравился дизайн и цветовая гамма 🥰👍
ردحذف👍
ردحذفHii cm Bei yake ni sh ngapi
ردحذفWanauza 650,000/=
حذف650,000/= tu
حذفTheirhr
ردحذفUrisyei
ردحذفUrisyei
ردحذفTembelea kurasa za Infinix Mobile Tanzania kufahamu zaidi
ردحذفHii CM bei gani inauzwa? Na duka lipo wapi?
ردحذفHow much is sold
ردحذفإرسال تعليق