INFINIX TANZANIA, YADOKEZEA UZINDUZI WA NOTE 30 SERIES .



Infinix Tanzania yaashiria ujio wa simu mpya nchini, tayari kampuni hii ya simu za mkononi imetupia picha mtandaoni uliombatana na ujumbe unaosema “Nambari Uno, unajua feeling ya kuwa namba moja wewe, tunakuja kubadilisha mtazamo kwenye Wireless charging #infinixmobiletz #NOTE30Series #SpidiKasi #comingsoon.”

Habari nyepesi nyepesi kutoka ndani, Infinix NOTE 30 kuzinduliwa katika hotel ya nyota 5 miongoni mwa wageni waalikwa ni wafanya biashara, kiongozi wa serikalini pamoja na wasanii wa Music wa kizazi kipya akiwemo Marioo na wengineo.

Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali inasemekana Infinix NOTE 30 series kuja na mfumo wa wireless chaji lakini pia inauwezo wa kugawa chaji kwa simu nyengine kupitia wireless pot lakini pia inasemekana teknolojia yake ya fast chaji ya wat68 + 50wat inajaza simu chaji kufikia asilimia 80 kwa muda wa dakika 30 tu hadi sasa ni simu pekee duniani yenye uwezo huu ambayo itapatikana duniani kote kwa gharama nafuu.


huku wakiwa wanatarajia kufanya kazi na app maarufu kwa sasa ya watumiaji wengi sana duniani TIKTOK, infinix inakupa nafasi kila mtu wa kila rika kufurahia simu hii kwa namna tofauti, hivyo basi kama wewe ni mtumiaji wa app hii ya TikTok pia niwakati wako kushinda na kutumia simu hii Infinix note 30 chakufanya endelea kukaa karibu na kurasa zetu ili kuweza kujua unapate simu hii kupitia TIKTOK.


Kuhusu bei na sifa nyengine za simu hii tembelea @infinixmobiletz

Post a Comment

أحدث أقدم