TEKNOLOJIA YA FAST CHAJI KWENYE SIMU ZA INFINIX NOTE 40 SERIES INAVYOENDELEA KUJICHUKULIA UFALME

Katika ulimwengu wa simu za mkononi ambao ni wa ushindani mkubwa kuwa mbele ya mpinzani wako ndio kitu pekee kitakupelekea kuwa bora, tukiangalia baadhi ya matoleo ya Mwaka huu wa 2024 tunaona namna ambavyo makampuni ya simu yalivyowekeza kwenye teknolojia mfano mzuri wa matoleo haya ni Samsung A55, Infinix Note 40 na Xiaomi Note 13.

Kupitia Makala hii utapata kujua ni wapi Samsung wameboresha kwenye series ya A55 na ni wapi Infinix na wamefudhu kwenye toleo la NOTE 40.

 

Tuanze kwa kuangalia Matoleo ya simu za NOTE 40, toleo ambalo linajumuisha NOTE 40, NOTE 40 Pro na NOTE 40 Pro+ 5G. Sera kuu iliyotumika kufikia wateja wake ni Uharaka wa simu hizi kupokea Chaji kupitia Wire na Pasipo Wire ‘TakeCharge24/7’ ikimaanisha popote pale uwe katika miangaiko, mazingira yenye hali ya baridi kali basi huna haja ya kuwa na hofu endapo unatumia moja kati ya simu hizi za NOTE 40, NOTE 40 Pro au NOTE 40 Pro+ 5G.

NOTE 40 series zinakuja na vifaa ambavyo vinapitisha nisharti ya umeme kwenda kwenye battery la simu kwa haraka, kulinda charge isipungue kwa haraka na kutoa ulinzi wakati wa kucharge teknolojia hii kitaalamu inafamika kama All Round FastCharge 2.0.

All Round FastCharge 2.0 ya NOTE 40 Pro+ 5G uruhusu kuchaji kwa wire na kwa ufanisi kwa Watt 100 na hukupa hadi asilimia 50% za nisharti kwa dakika 8 na kwa kutumia wireless Magpower kupitisha charge kwa ufanisi kwa Watt 20.

Muongoza mzima wa ufanyaji kazi katika mifumo ya charge ‘All Round FastCharge 2.0’ katika simu hizi unatokana na usimamizi hodari wa Chip ya Cheetah X1, Chip iliyojitengenezea Infinix katika simu za Note 40 series pamoja na kuchaji kwa kasi pia inasimamia kuchaji kwa Bypass na Ulinzi wa kuchaji kwa AI, kugawa charge kwa kugusanishaji Note 40 na kifaa chengine chenye wireless.

 

Tukiangalia upande wa Samsung A55 tunaona uwekezaji kwenye muonekano na utendakazi. Simu za A55 zinatumia chipset ya Exynos 1480 na nano 4 hii inatoa kasi kubwa ya utendaji ikilinganishwa na matoleo ya awali, ikiboresha uzoefu wa mtumiaji na kufanya kazi ya simu kuwa haraka zaidi na laini.

Teknolojia ya nano 4 inaboresha ufanisi wa nishati, ikisaidia kuongeza Maisha ya betri na kupunguza uishaji wa chaji kwa haraka iliyopitishwa na fast charge ya Watt 25.

Hayo ndio mabadiliko makuu yaliyofanywa na kampuni ya Infinix pamoja Samsung katika simu zao za daraja la kati pasipo kusahua boreshwa la Android simu zote zinatumia Android 14.


Feature nyengine ambazo zimekuwa advertised mitandaoni tukianza na Samsung ni design yenye material ya gorilla Glass na ukubwa wa kioo inch 6.6 AMOLED display, camera 3 nyuma 50MP+12MP+5MP pamoja na uwezo wakuchukua video kwa 4K na kwa upande wa Infinix Note 40 series ni muundo wa 3D curved 6.7 AMOLED display Gorilla glass, Camera 3 nyuma 108MP+2MP+2MP na Mediatek Dimensity 7020.

Kwa ufupi Infinix imefanya kile ambacho wengi hatukufikiria kukiona kwenye simu za daraja la kati teknolojia ya All Round FastCharge na wireless magnetic charge kabla ya hapo imekuwa kwenye simu kama iphone 15 series ambapo bei zake ni juu ilihali Infinix imeweka record ya kwanza kuwa na feature hii na kupatikana kwa bei nafuu.


#TechLazima

 



7 تعليقات

إرسال تعليق

أحدث أقدم