Na Mwanahabari wetu
Juhudi zingine za kipekee ambazo zinaenda kuleta mapinduzi za smartphone nchini Tanzania, Kampuni ya infinix imebainisha toleo lake jipya la simu iitwayo Hot 50 Pro Plus. Hii ni hatua ya kipekee ambayo imewavutia wengi ndani na nje ya sekta ya mawasiliano kwa sababu simu hii inasadikika kuwa simu nyembamba zaidi duniani yenye unafuu wa bei.
Muundo wa Hot 50 Pro Plus utalenga katika kuongeza wembamba kwa kuunganisha pamoja simu ya Infinix’s high tech ambayo ni maarufu kwa uwezo wake wa utendaji wa kiwango cha juu na wembamba wake ambao haujawahi kuonekana hapo awali. Simu hii inaambatanisha mali ghafi za kisasa na za ubora wa kiwango cha juu na mtindo wa kisasa zaidi kwa lengo la kudumisha uimara na utendaji wake wakati huo huo ikiwa na umbo jembamba na wepesi ambao hakuna simu nyingine imewahi kufikia.
@infinixmobiletz amethibitisha kwamba uzinduzi huu ambao
unatarajiwa kufanyika nchini Tanzania Jumamosi yah ii, utaambatana na matukio
ya kipekee ikiwemo ushirika wake na Boomplay ambao unalenga kumpa burudani
kijana kupitia Nyanja ya music ikiwa ndio lengo moja wapo la Infinix kumfikia
kijana kupitia burudani, mitindo na technolojia.
Uchambuzi wa soko unaashiria kuwa simu ya Hot 50 Pro
Plus italeta mapinduzi makubwa ya muundo wa simu za smartphone na mfano wa
kuigwa na makampuni mengine.
Tembelea @infinixmobiletz kwa taarifa zaidi.
إرسال تعليق