Umewahi kuwa unacheza games, kuangalia movie au kuperuzi mtandaoni na ghafla simu ikakutaarifu kuwa na chaji kidogo ukaamua kuiweka chaji huku ukiendelea na kile ulichokuwa unakifanya bila kuwaza kuwa hicho kitendo kinaweza kuwa na madhara?
Fahamu madhara yanayoweza kutokea ukitumia simu wakati unachaji;
•Kuvimba/Kupasuka betri ya simu yako.
•Kupelekea uvujaji wa kemikali kemikali hatari za betri.
•Kupelekea simu yako kutokuwaka.
•Inaweza kupelekea Hadi madhara makubwa zaidi kama kifo.
> Mwaka 2013 huko Thailand Mwanaume aliripotiwa kufa wakati anachaji na kutumia simu.
> Mwaka 2013 hiyo hiyo mwanamke china aliripotiwa kufa akitumiwa simu wakati anachaji.
> Mwaka 2014 mtoto wa Miaka kumi alijeruhiwa wakati akitumia na kuchaji simu kwa wakati mmoja.
Kwa matukio yote hayo hapo juu watumiaji walikuwa wanatumia simu za iPhone.
Japo kwa sasa simu nyingi zimejitahidi kuongeza usalama kwenye simu kwa kuweka safe mode lakini tunashauriwa kutotumia simu wakati inachajiwa.
#TechLazima
Chapisha Maoni