INFINIX NA SIMU YA KWANZA DUNIANI WIRELESS KWENYE RANGE YAKE

 

Infinix Note 30 Pro, ni simu ya hali ya kisasa na bora iliyozinduliwa hivi karibuni na kampuni ya Infinix, simu hii inakuja na sifa bora ambazo ni pamoja na Teknolojia ya Fast Charge Watt 68, Wireless Fast Charge Watt 15, kioo cha AMOLED, kamera yenye nguvu ya 108MP, uhifadhi mkubwa pamoja na battery yenye kudumu na chaji kwa muda mrefu.

Kupitia makala hii tutaenda tutapata kuifahamu Infinix NOTE 30 Pro kiundani zaidi.

Fast Chaji yenye Spidi



Simu hii ina betri ya Li-Po yenye uwezo wa 5000 mAh, ambayo inafanya simu yako kudumu na chaji siku nzima bila kuchaji. Pia kama unahitaji kuchaji simu yako kwa uharaka, Infinix Note 30 Pro inakuja na teknolojia ya fast charging ya hadi 68W, ambayo inaweza kuchaji betri ya simu hiyo hadi asilimia 80 ndani ya dakika 30 tu.

Pia, Infinix Note 30 Pro inakuja na teknolojia ya wireless charging ya 15W ambayo pia inaweza kufanya simu hiyo kuchaji simu nyingine kwa kutumia wireless.

Kioo cha AMOLED



Infinix Note 30 Pro inakuja na kioo cha AMOLED chenye ukubwa wa inchi 6.78. Kioo hiki kinaonyesha rangi zenye kina, huku kikiwa na uwezo wa kuonyesha rangi zaidi bilioni 1 kupitia resolution ya 1080 kwa 2460 pixel. Utaweza kungalia video na picha kwenye mitandao ya kijamii kwa upana kwani kioo hichi ni kipana na kisichokuwa na kingo kubwa yaani Full Display.

Kamera yenye Nguvu



Moja kati ya sifa kubwa ya Infinix Note 30 Pro ni mfumo wake wa kamera ambapo inakuja na kamera tatu za nyuma huku kamera kuu ikiwa na Megapixel 108MP huku ikisaidiwa na kamera ya pili ya 2MP, na kamera ya tatu ya QVGA.

Hii inamaanisha kuwa unaweza kupiga picha zenye muonekano mzuri na zenye details zaidi hasa kama wewe ni mtumiaji wa mitandao ya kijamii, mtumiaji wa kawaida au hata kama wewe ni mfanyabiashara wa mtandaoni.

Kamera hizi zinakuja na flash ya Quad-LED, HDR, pamoja na panorama, na pia zinaweza kurekodi video za hadi 1440p@30fps au 1080p@30fps. Kwa upande wa selfie Infinix Note 30 Pro ina kamera ya mbele ya 16MP na flash ya LED, hii itakusaidia kuhakikisha kupata picha bora hata katika mwangaza hafifu.

Utendaji Imara



Infinix Note 30 Pro inatumia chipset ya Mediatek MT8781 Helio G99 (6nm), pamoja na CPU ya Octa-core yenye kasi ya 2.2 GHz Cortex-A76 na 2.0 GHz Cortex-A55. Hii inamaanisha kuwa simu hii ina nguvu ya kutosha kufanya mambo mbalimbali kama vile kwa wapenzi wa game, na kazi nyingine kama kuedit video, picha na kutumia programu nyingine bora. Kupitia GPU ya Mali-G57 MC2 inaboresha uwezo wa kucheza Game na inahakikisha picha, na video zinaonekana kwa urahisi na kwa ubora mzuri.

Uhifadhi Mpana



Infinix Note 30 Pro inakuja na machaguo ya uhifadhi wa ndani wa GB 128 au GB 256. Hii inamaanisha kuwa utakuwa na nafasi ya kutosha kwa faili zako zote, kama picha, video, na programu mbalimbali. Mbali na hayo pia kama haitoshi utaweza kuongeza uhifadhi wa ndani kwa kutumia Memory Card yenye uwezo wa hadi GB 512..

Muundo wa Kuvutia



Infinix Note 30 Pro inakuja muundo mzuri na rangi za kuvutia za Magic Black na Variable Gold, ambazo zinafanya simu hii iwe na muonekano bora na wa kuvutia. Mbali na hayo simu hii pia ina sensori ya alama ya vidole kwa upande, ambayo ina kuhakikishia usalama kwenye kifaa chako.

Pamoja na hayo Infinix Kuungana na TIKTOK haijawaacha nyuma watumiaji wake na kuendelea kugawa zawadi kila kona. Msimu huu nikwaajili ya kila mtu kama wewe ni mtumiaji wa TIKTOK unanafasi ya kushinda simu INFINIX NOTE 30 mpyaa kwa kutumia App hii chakufanya record video yako ukiwa unanyesha kipajichako kwa kutumia filter ya infinix (TakechargewithNote30) na record kabla alama ya chaji haijajaa onyesha ubunifu wako huku ukitumia #TakechargewithNote30 na watag @InfinixmobileTz na ujishindie Simu yako mpyaa kabisa.

Hitimisho

Kwa ujumla, Infinix Note 30 Pro ni simu ya kuvutia na yenye sifa bora zaidi. Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanatafuta simu bora kwaajili ya matumizi ya kuchukua picha na video bora kwaajili ya mitandao ya kijamii, au kwaajili kupiga picha bora kwaajili ya biashara yako basi simu hii ni chagua bora sana. Pia kwa wapenzi wa Game pamoja na kutumia Apps mbalimbali simu hii pia inakuja na uwezo mkubwa sana kwaajili ya matumizi hayo.

Pia Kumbuka kuwa #Gusanishaijae ndio hashtag ya kutumia kwani simu hii inakuja na teknolojia ya kuchaji simu nyingine kwa kutumia mfumo wa Wireless. Yaani unaweza kuchaji simu nyingine kwa kuweka simu yako juu ya Infinix Note 30 Pro. 

Wasiliana nao 0745170222 wakupe maujanja zaidi.


#TechLazima

11 Maoni

  1. Вауууу, телефон Infinix Note 30 Pro - самое лучшее что я видел ,а больше всего понравился дизайн и цветовая гамма 🥰👍

    JibuFuta
  2. Hii cm Bei yake ni sh ngapi

    JibuFuta
  3. Tembelea kurasa za Infinix Mobile Tanzania kufahamu zaidi

    JibuFuta
  4. Hii CM bei gani inauzwa? Na duka lipo wapi?

    JibuFuta
  5. How much is sold

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi