Ulimwengu ukiwa bado kwenye wimbi la toleo lililopita la Reno 6 ambayo ina support 5G ni tetesi na uvumi unao endelea kuzungumzwa tayari Oppo inatarajia kutoa Reno series nyingine ambayo ni Reno 7 na Reno 7 pro.
simu hizi mbili zinazo endana na kupishana kitu kidogo tayari zimezua mzozo ulimwengu wa makampuni ya simu. Oppo Reno 7 inatarajiwa kuwa na uendeshaji wa Mediatek Deminsity 1200 SoC inayooanishwa na 8GB ya Ram.
Uzinduzi wa mfululizo wa Oppo Reno 7 unaonekana kukaribia kwani Oppo Reno 7 Pro sasa imeonekana kwenye tovuti ya kuweka alama ya Geekbench. Orodha hiyo inapendekeza kwamba simu mahiri inayokuja itaendeshwa na MediaTek Dimensity 1200 SoC iliyooanishwa na 8GB ya RAM. Kando, picha imeibuka mtandaoni inayoonyesha muundo wa paneli ya nyuma ya vanilla Oppo Reno 7 inayokuja. Msururu huo unatarajiwa kuzinduliwa nchini China mwezi huu.
Kitu ambacho wameweza kukibadilisha na ambacho ni chakipekee ni Umbo na ujio wa mwonekano mpya wa Camera ya simu hii, Tangu simu zianzishwe kwenye kampuni ya Oppo haijawahi kua na muonekano wa kamera hii.
kaatayari kupokea ujio mpya wa Oppo kwa upande wa Reno series na Ujionee maajabu kwenye Simu hii, na pia kama unahitaji kufahamu zaidi juu ya simu hii tafahdali endelea kutembelea page za zoom tech kwa Updates zaid.
TechLazima.
Chapisha Maoni