Dar-es-Salaam, 14-12-2021; Kampuni ya simu Infinix imetangaza simu mahiri mpya aina ya Infinix HOT 11 na HOT 11 play ikishirikiana na kampuni ya mawasiliano Tigo.
Kwa mujibu wa Afisa wa Uhusiano Infinix, Aisha Karupa alisema, “Infinix HOT 11 na Infinix HOT 11 play ni matoleo ya kwanza ya series ya HOT kuja na memory yenye ukubwa wa GB 128 na Ram ya GB4, Infinix tumezingatia zaidi uhitaji wa kuhifadhi kumbukumbu za mteja wetu katika hali ya usalama hasa katika karinee hii ambayo watanzania wengi mawazo yetu yamepanuka kwa ukubwa na tunaitumia simu kama sehemu yetu ya office”,
baadhi ya sifa nyengine ambazo zimetajwa na Bi Aisha hadi kupekelea kuzipa jina la simu za funga mwaka amezitaja kuwa ni, “battery ya mAh6000, kamera tatu nyuma kamera kuu ikiwa na Megapixel 50 pamoja na flash mbili na kusisitiza model zote mbili zinaweza kuchukua picha hata katika wakati wa usiku lakini pia ni simu zenye kuonyesha matukio kupitia kioo cha simu hiyo kwa uzuri zaidi kutokana na ukubwa wa kioo cha inch6.82 na resolution FHD +”.
Meneja biashara Tigo, Suleimani Bushagama akizungumza wakati wa uzinduzi huo alisema, “Ushirikiano wetu na Infinix ni wa kujivunia kwa sababu unaendana vyema na maono yetu ya kuleta ulimwengu mpya wa kidijitali kwa wateja. Uzinduzi huu wa aina nyingine ya juu zaidi, simu mahiri ya bei rafiki, ni uthibitisho wa dhamira yetu ya kuhakikisha kwamba kila mtu anafurahia manufaa ya maisha ya kisasa yaliyounganishwa kupitia huduma na bidhaa tunazotoa vile vile Tigo tunatoa ofa ya GB 76 za internet kwa wateja wote wa Infinix HOT 11 na HOT 11 play”.
Infinix HOT 11 play inapatikana katika maduka yote ya simu nchini Tanzania zikiambatana na zawadi mbalimbali za msimu huu wa sikukuu ya Christmass na Mwaka mpya.
Zoom Tech inaendelea kukupa taarifa za kila wakati kiganjani mwako endelea kutembelea page na kurasa zote za zoom tech kwa taarifa zaidi.
Tech Lazima
Shingap
JibuFutaTunashukuru tigo Kwa kutuhamasisha
JibuFutaZnapatikana kwa shilingi ngapi?
JibuFutaIvi hii offer mbona mm siipati
JibuFutaChapisha Maoni