Kampuni ya Infinix imeendelea kufanya vizuri na kukimbiza soko la simu janja hapa Tanzania ambapo sasa imekuja na simu aina ya Infinix HOT 12 yenye sifa kem kem zilizoifanya kampuni ya sumsung kubaki na sintofahamu.
Sasa Sumsung imekuwa ikikumbana na changamoto tokea kampuni ya Infinix imeanza kutoa matoleo yake ambayo yamekuwa yanakuja na uwezo wa kuipa challenge Samsung ambayo imekuwa ikifanya vizuri kabla ya infinix kuja na kasi ya kutoa simu zenye ubora na specifications nyingi na kubwa zaidi.
Tuchambue pamoja hatua kwa hatua ukubwa wa simu yao mpya aina ya Infinix HOT 12;
1. PROCESSOR
Mfumo wa uendeshaji wa toleo jipya la Infinix HOT 12 ni mkubwa zaidi ukilinganisha na Samsung A13, Infinix HOT 12 imeweza kurahisisha matumizi ya simu na kazi kwa ujumla maana unaweza kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja huku ikitoa nafasi kubwa kwa wapenzi wa kucheza games kuweza kufurahia kasi yake, Processor yake ambayo ni MediaTek Helio G85 inaipa nguvu simu ya Infinix HOT 12 kiutendaji huku simu ya Samsung A13 ikiwa na processor ndogo ukilinganisha na Infinix HOT 12, processor yake ni ya Exynos 850.
Infinix ina 90Hz refresh rate inayoipa wepesi zaidi simu kufunga na kufunga mafaili pamoja na kuonesha kwa uzuri zaidi huku Samsung A13 ikiwa na 60Hz refresh rate inayoifanya kuwa slow kulinganisha na Infinix HOT 12.
2.SOUND
Kwa upande wa speaker simu ya Infinix HOT 12 imekuja na speaker mbili zinazokupa experience ya khali ya juu unaposkiliza chochote kwenye speaker zake huku simu ya Samsung A13 ikiwa na speaker moja tu.
3.STORAGE
Infinix HOT 12 ina storage ya 128GB na ram ya hadi 7GB kuipa nguvu na nafasi ya kutosha simu huku ikitoa nafasi ya kuifadhi mafaili yako bila wasi wasi lakini pia kuyafungua utakavyo bila kikomo kwa maana ram ni kubwa, kwa upande wa Samsung A13 ina ram ya 6GB kufanya izidiwe uwezo wa ram na Infinix HOT 12.
4.BATTERY
Simu zote hizi zina betri sawa 5000mAh, huku Infinix HOT 12 ikiwa na 18W fast charging kuizidi Samsung A13 yenye 15W fast charging. Kwa mujibu wa watumiaji wa simu hizi mbili Simu ya Infinix HOT 12 imekuja na matokeo ya kukaa na chaji mda mrefu zaidi.
5. BEI
Simu ya Infinix HOT 12 inapatikana kwa Tsh. 450,000/= huku simu ya Samsung A13 ikipatikana kwa bei ya kuanzia Tsh. 500,000/= na kuendelea pamoja na kuwa na specifications zilizozidiwa na Infinix HOT 12.
UPATIKANAJI
Infinix HOT 12 inapatikana sasa madukani kote nchi nzima nje na ndani ya Dar es salaam ambapo kwa sasa wanatoa zawadi kwa wateja wake watakao nunua simu hii.
Je ungependa tuongelee simu gani kwenye mada inayofuata? acha pendekezo lako hapo kwenye comment section nasi tutalifanyia kazi.
Zoom Tech Team.
.jpg)


Chapisha Maoni