INFINIX Hot 12 NA INFINIX Hot 12 Play ZATUA NCHINI TANZANIA.

Simu aina ya Infinix HOT 12 imezinduliwa rasmi nchini Tanzania, kampuni ya simu Infinix imezingatia swala la speed na chaji kwenye simu hii janja. Tayari simu hii iko sokoni na hizi zimetajwa kuwa sifa za kipekee kuwahi kuwepo kwenye matoleo ya awali ya series ya HOT, processor Mediatek Helio G85, fast charji usb type c ya watt 18, kioo cha inch 6.82HD+ na refresh rate ya nyuzi 90Hz pamoja na teknolojia ya touch rate ya nyuzi 180.


Infinix HOT 12 inauwezo wa kuendesha aina yoyote ya game, katika uzinduzi huo afisa wa Uhusiano Infinix Aisha Karupa aliyasema haya, “Tunafuraha kuzindua Modeli ya kwanza ya Infinix kutoka mfululizo wa HOT itakayokuwa na chipset ya G85 ya games, Infinix Hot 12 ni simu bora na nyepesi zaidi kwa upande wa game ambapo mtumiaji anaweza kucheza game lake bila kugandaganda na huku akiendelea kuwasiliana katika mitandao mingine ya kijamii n.k , lakini pia ina ubora wa juu zaidi wa  betri, Infinix HOT 12 ina vifaa vya 5000mAh, chaji ya hali ya juu ya Type -C18W, teknolojia ya kudumu ya betri ya Infinix iliyojitengenezea ambayo hufanya betri ikae na chaji kwa muda mrefu sana, ambapo chaji 5% inaweza kukaa na kutumika kwa hadi masaa 2.6 ”




Bwana Blass Abdon kutoka Tigo Tanzania na Afisa Uhusiano Infinix Aisha Karupa wakizindua simu hiyo


"Infinix HOT 12 ina mwonekano wa kuvutia na skrini ya inchi 6.82" ya 90Hz Pro-Level ya esports kwa ingizo laini la silky-laini na sampuli ya mguso 180Hz inayoipa Infinix HOT 12 kiwango cha mwitikio cha haraka ambacho ni bora kabisa kwa games. Infinix HOT 12 sasa inapatikana katika maduka yote ya simu nchini Tanzania ikiwa na ofa ya GB78” aliongeza Aisha Karupa.


 Mambo yanayo endelea kwa kampuni za simu za mkononi ni ushindani na kila mmoja yuko kutoa na kuhakikisha ana kidhi mahitaji ya watumiaji wake infinix Mobile TZ imekua ikihakikisha kutoa mahitaji ya watumiaji ipaswavyo kwa kutoa simu nzuri na za bei nafuu ambazo kwa watanzania wote wa vipato vyote wanaweza kutumia simu hizi.


Infinix hot 12 ni simu ambayo imekuja kutikisa soko hili kwani ina ka muonekano flani ivi ambao baada ya uzinduzi huu watu wengi wamesema wataitumia na kuinunua, baada ya uzinduzi huu wa simu hii wengi wamevutiwa na vitu ambavyo viko ndani ya simu hii.


Fura yetu sisi kama waandishi nikuona makampuni yanakidhi mahitaji ya watumiaji na nilengo letu kuwaletea kitu ambacho nikizuri na kina faa kwa mahitaji ya kila siku.


endelea kufuatilia kurasa za ZOOM TECH ili kuwa wakwanza kupata habari zote mpya juu ya ulimwengu wa kiteknolojia.

 


Tembelea @infinixmobiletz au piga nambari ya simu 0743558994 kwa huduma ya haraka.


#TechLazima

 


 

 

 


Post a Comment

Mpya zaidi Nzee zaidi