Apple imetambulisha mfumo mpya wa iOS 16 ambao utatoka kwa watumiaji wa iPhone 8 mpaka iPhone 13 zote.
Mfumo mpya wa iOS 16 itakuwa na muonekano mpya; itakuwa na option ya kubadili text za kuonyesha muda, rangi ya Lock Screen, kuweka widgets katika Lock Screen, na notifications zitakuwa zinajipanga kwa upande wa chini.
Mabadiliko haya yakianza, watumiaji watakuwa na option ya kuchagua muonekano wa Lock Screen kuendana na wanavyotaka wao. Mfumo mpya unategemewa utatoka mwezi wa 9 au mwezi wa 10. Kwa Developers tayari mfumo wa majaribio (Beta) umetoka na kwa Public Beta itatoka mwezi ujao.
Haya ni mabadiliko ambayo yamekwepo kwa watumiaji wa Android kwa muda mrefu! Katika mfumo wa Android ni rahisi sana kubadili muonekano wa Lock Screen, rangi, aina za maandishi n.k.
Vipi unaonaje muonekano mpya wa Lock Screen ya iPhone?

.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
Chapisha Maoni