Mazoea Yalivyopelekea Kununua Samsung A14 na Kujutia kisa Infinix NOTE 12

 

Ndugu zangu naomba tulijadilini hili nimekutana nalo huko kwenye pitapita zangu nanukuu,


“Nimejichanga ili kununua simu mpya na nzuri nikaenda sokoni kariakoo nikajinunulia Samsung A14 mwanzo nilikuwa nafikiri Samsung ni brand kubwa kwahiyo lazima niwe na simu ya hii brand, sasa nimetumia simu hii kwa takriban miezi michache, nimegundua kuwa iko speed kama nilivyofikiria, kwangu simu ni kifaa muhimu sana naperuzi sana mtandaoni, gaming na documentation lakini simu hii hainipi kasi niliyotarajia. saa zingine nilikuwa nacheza eFootball na inastack ikiwa nakaribia kufunga bao inabidi ianze upya na chaji pia kero muda wote niko na power bank, labda G80 yake haifanyi kazi vizuri baada ya kurudi niliponunulia wamesema hata kuhama kutoka app moja kwenda nyingine wakati wa kufungua app nyingi zinafunguka kwa shida, nikawa natamani simu yenye processor ya utendaji wa juu haswa.


Linganisha na jirani yangu alijinunulia Infinix Note 12 kwa bei kama sawa na Samsung A14 lakini ilikuwa na processor zaidi ya yangu na inakaa na nguvu tena yeye huwa anajisifu juu yake, nilianza kuhisi ningekuwa na furaha pia na simu hiyo kulinganisha na yangu, wasiwasi wangu ulikuwa kwenye vifaa akanitoa hofu maana tukija kwa Samsung vifaa vyake vinapatikana kwa wingi japo ni bei ghali ila uhakika kuvipata popote”.


Hapa nauliza mimi kama mimi, Je wewe ni changamoto gani ulikutana nayo kwenye simu yako ya awali na ni nani amekushawishi kununua simu mpya


#TechLazima

9 Maoni

  1. Mimi nakubaliana na wewe, Natumaini NOTE 12 VIP Iko vizuri balaa

    JibuFuta
  2. Bei yake?

    JibuFuta
  3. nahitaj, Ntaipata wapi?

    JibuFuta
    Majibu
    1. utapata tupigie 0743558994

      Futa
  4. Kwenye hizo A series nakubaliana na wewe, Ila S series Samsung wako vizuri

    JibuFuta
  5. Zipo hizo?

    JibuFuta
  6. Bei Gani?

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi