INFINIX HOT QUIZ DIT KIDEDEA, UDSM, CBE NA IFM CHALI

 


Wanafunzi wa chuo kikuu DIT waibuka kidedea baada ya kivipiga chini USDM, CBE na IFM kupitia shindano la maswali na majibu ya kiteknolojia shindano ambalo limeandaliwa na kampuni ya simu za mkononi Infinix.



Kwa takribani week nne mfululizo DIT imekuwa ikishikilia nafasi ya kwanza na hadi kuibuka washindi ambapo Mzamini mkuu wa mashindano haya kampuni ya simu Infinix ilikabidhisha simu aina ya Infinix HOT 30 kwa washiriki wote wa chuo cha DIT.

Infinix imewapongeza wanafunzi wote kwa kushiriki katika kipindi hicho cha Tech kwa kuonyesha uhodari wao katika swala zima la teknolojia, ikiwa kama kampuni yenye kujali maendeleo ya kijana si mara ya kwanza kampuni hii imeshirikiana kwa ukaribu na vijana, tukirudi nyuma kupitia series hii hii ya HOT Infinix iliandaa mashindano ya mpira wa miguu kwa vijana wa chuo na mtaani ambapo vijana wa Temeke walijishindia Infinix HOT 12.

#TechLazima

12 Maoni

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi