INFINIX KUJIVUNIA NOTE 30 PRO ALL ROUND FAST CHAJI, 108 CAMERA PIXEL.

Mitandao nguli ya tech duniani kote imeisifu vikali kampuni ya simu za Mkononi Infinix kwa uthubutu huu wa kuja na teknolojia ya wireless reverse fast charge, haijaishia hapo NOTE 30 Pro ni tishio kwa simu nyingine zenye kima sawa cha bei, tangu kuzinduliwa kwakw popote pale kwenye soko la simu kwa nchini Tanzania wimbo ni nahitaji Infinix NOTE 30 au NOTE 30 pro au NOTE 30 Vip.

Samsung A34, TECNO Camon 20 Series ni miongoni mwa simu ambazo huenda zimeathiriwa na ujio wa Infinix NOTE 30 Series, pamoja na kwa karibu tuangalie tofauti kati ya Infinix NOTE 30 Pro na Samsung A34 kifeatures na bei.

Kamera



Kwenye idara ya picha, Note 30 Pro pia inaonekana kuwa bora zaidi kwani ina mfumo wa kamera kuu ya 108 MP pamoja na kamera ya kina ya 2 MP na kamera ya makro ya 2 MP, na kamera ya selfie ya 32 MP. Hii ni tofauti kubwa kutoka kwa mfumo wa kamera ya Galaxy A34 yenye MP 48 na kamera ya selfie ya MP 13. Kwa Note 30 Pro, watumiaji wanaweza kutarajia picha zenye rangi nyingi na muonekano bora zaidi.

Teknolojia ya Fast Charge



Simu zote mbili zina betri yenye uwezo wa 5000 mAh, ikitoa nguvu ya kutosha kwa matumizi ya siku nzima. Hata hivyo, Note 30 Pro inaongoza na uwezo wake wa fast charging ya hadi 68W.

Mbali ya hayo Infinix Note 30 Pro inakusogezea ulimwengu mpya #GusainishaIjae ambapo sasa simu mpya ya Infinix NOTE 30 Pro inakuja na uwezo wa kuchaji simu nyingine kwa kugusanisha na simu ya nyingine yenye wireless charging. Sehemu hii husaidiwa na teknolojia ya reverse wireless charging yenye uwezo wa hadi 15W.

Kwa upande mwingine simu ya Galaxy A34 inakuja na fast charging ya 25W. Huku ikiwa haina teknolojia ya kuchaji simu nyingine. Hii inafanya Infinix Note 30 Pro kuchaji kwa haraka ndani ya muda mfupi, ambao ni faida kubwa kwa wale ambao wana haraka ya kupambana na Maisha.

Kioo



Infinix Note 30 Pro ilitangazwa tarehe 16 Mei 2023, na kuja na huduma kadhaa muhimu. Ina kioo kikubwa cha inch 6.78 AMOLED, kikiwa na resolution ya FHD+ yaani pixel 1080 kwa 2460, kioo ambacho ni kubwa kuliko kioo cha Samsung A34 chenye inch 6.6. Kioo cha Note 30 Pro pia kinakuja na refresh rate ya juu ya 120Hz ili kusaidia kutumia apps na game kwa urahisi zaidi.

Utendaji



Kwa utendaji, Infinix Note 30 Pro inatumia processor ya MediaTek Helio G99 ultra-power, iliyotengenezwa kwa teknolojia ya 6nm, na kasi ya processor inayofikia 2.2 GHz. Hii inaambatana na RAM iliyozidishwa hadi 16GB na uhifadhi wa 256GB.

Kwa upande mwingine, Samsung A34 inatumia chipset ya MediaTek MT6877V Dimensity 1080 yenye CPU ya octa-core na inatoa hadi RAM ya 8GB na uhifadhi wa 256GB. Note 30 Pro inazidi kuwa bora kutokana na uwezo wake wa RAM wa juu, hivyo uwezo huu utafanya uweze kutumia simu hii kwa haraka zaidi kuliko Galaxy A34.

Kwa upande mwingine simu ya Galaxy A34 inakuja na fast charging ya 25W. Huku ikiwa haina teknolojia ya kuchaji simu nyingine. Hii inafanya Infinix Note 30 Pro kuchaji kwa haraka ndani ya muda mfupi, ambao ni faida kubwa kwa wale ambao wana haraka ya kupambana na Maisha.

Bei

Bei ni moja kati ya sehemu muhimu kuangalia hasa kama unataka kununua simu kwa mwaka huu 2023, kwa upande wa bei Galaxy A34 inapatikana kwa bei ya kuanzia TZS 700,000 bei hii inaweza kuongezeka kulingana na mahali utakapo nunulia simu hiyo, huku kwa Infinix Note 30 Pro unaweza kupata sifa zote ikiwa na mfumo wa #GusainishaIjae kwa TZS 650,000 Tu.

Watembelee @infinixmobiletz #Samsung au piga 0745170222.

2 Maoni

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi