Kampuni ya simu za mkononi Infinix yenye makao makuu nchini Hong Kong yatwaa ushindi katika usanifu wa bidhaa/vyombo vya habari na electroniki za nyumbani nchini Paris. Hapo jana Infinix Tanzania kupitia kurasa zake za mtandao wa kijamii @infinixmobiletz ilipost video kusherehekea ushindi huo uliopatikana kupitia simu mahiri aina ya Infinix NOTE 30.
Infinix NOTE 30 ilifanikiwa kuwagalagaza washindani wenzake kutoka makampuni mbalimbali ya simu na kutwa taji katika kipengele cha ubora wa muundo wa simu kwa Mwaka huu 2023, hii si mara ya kwanza Infinix kujitwalia Tuzo hizi za kimataifa Mwaka 2022 ilijishindia Tuzo za Asia katika kipengele cha mawasiliano kupitia simu aina ya Zero Ultra.
Tuzo hizi za mara kwa mara zinathibitisha ubora kwa kampuni hii, kwa kuingalia Note 30 si simu yenye muda mrefu sokoni lakini ubunifu mkubwa uliofanyika katika utengenezaji wa simu hii umeipa heshima kubwa Infinix ulimwenguni kote.
Tutegemee makubwa kutoka kwao kasi yao katika uzalishaji wa simu zenye teknolojia ya hali ya juu si yakubeza, Infinix si hodari tu kwenye designing wako vyema pia na teknolojia ya fast chaji na wireless chaji. NOTE 30 VIP ina fast chaji ya WATT 68 na wireless chaji ya WATT 50 pamoja na kureverse chaji ni moja kati ya simu za kampuni hii ambazo teknolojia ya fast chaji imewekezwa vyema ndani yake.
Tuzo za Usanifu wa DNA Paris huheshimu miundo katika taaluma za Usanifu, Usanifu wa Ndani, Usanifu wa Mandhari, Usanifu wa Picha na Muundo wa Bidhaa unaowatunuku wabunifu bora zaidi duniani kote.
Так держать 👍
JibuFutaВ общем и в целом я очень рад, что приобрёл телефон такой модели как infinix и очень надеюсь, что мы переплюнем айфон
JibuFutaChapisha Maoni