INFINIX ZERO 30 5G YAPENYA LEVEL ZA SAMSUNG.

 ZERO 30 5G ni flagship ya Infinix kwa mwaka huu wa 2023 na kati ya mabadiliko makubwa yaliyofanyika katika utengenezaji wa simu hii ni pamoja na camera ya mbele na nyuma kuwa na uwezo wa kuchukua video kwa mfumo wa 4k, 60fps, ongezeko la refresh rate hadi kufikia 144Hz na skirini ya Gorilla Glass 5 sifa ambazo tumezoea kuona kwenye flagship za Samsung kama S23 na nyinginezo.

Kutokana na mfanano wa baadhi ya features leo tutazichambua simu hizi mbili ‘Infinix Zero 30 5G na Samsung S23’ na kisha msomaji utafanya maamuzi ipi ya kununua kulingana na budget yako.



Camera Quality

Samsung Galax S23 imesalia kuwa mojawapo ya chaguo bora kwa wapiga picha tangu ilipozinduliwa mapema mwaka huu, kihisi/sensor chake kikuu cha Megapixel 50 nyuma na Megapixel 12 mbele vinaweza kuchukua picha nzuri chini ya hali yoyote. Infinix Zero 30 5G imeundwa ikiwa na kamera zenye uwezo zaidi kuonekana kwenye simu yoyote yenye gharama 1,060,000 kihisi chake kikuu cha nyuma ni Megapixel 108 na mbele ni Megapixel 50.

 

Video Quality

Simu zote mbili zinamfumo wa kisasa wa uchukuaji video. Katika hali yoyote camera zenye mfumo wa kuchukua video kwa 4K na 60fps video zake huonyesha kwa quality ya hali ya juu na uchezaji wa games za simu hutendeka vizuri. Mfumo wa kuchukua video kwa camera ya mbele ya Samsung ni 4k na 30fps na nyuma ni 8k na 30fps ambapo kwa Infiniz Zero 30 5G mfumo wake ni 4K na 60fps kwa kamera ya nyuma na mbele.

Kutokana na 60fps Zero 60 inauwezo zaidi katika uchukuaji video za slow motion.

 

Design.




Infinix Zero 30 kioo imekuwa moja ya feature kubwa katika kuitangaza ina AMOLED Display 6.78 inches lakini pia imetengenezwa pamoja na ulizi wa Gorilla Glass 5 upande wa mbele na nyuma. Galaxy S23 ina paneli za hivi punde nayo ni Gorilla Glass 2 Victus pande zote mbili. Panel za simu zote hizi mbili ni imara si nyepesi kuvunjika kirahisi wala kupata michubuko isipokuwa Victus 2 ni imara zaidi katika kipengele hiki.



Infinix Zero 30 5G ina refresh rate 144Hz na S23 ni 120, uonaji wa visual ni mzuri zaidi kupitia Infinix ZERO 30 5G na pia katika swala la kuperuzi ni smooth zaidi ya refreshrate 120Hz.

Kimuonekana wa maumbile simu zote zinavutia ni nyembamba na uzito wa kawaida zote zi kama zimepinda pembezoni hii ni style ya Samsung kwa kipindi chote cha matoleo ya S na sasa tunaiona design hii kwenye zero 30 5G.

 

Battery Life.

Galaxy S23 inaendeshwa na betri ya mAh 3900 na Watt 25 wakati Zero 30 ina seli kubwa ya mAh 5000 na Watt 68. Dakika tu 30 zero 30 inajaa chaji kwa asilimia 100 lakini pia imaisha marefu ya battery na Samsung huchukua dakika 59 kwa chaji kufikia asilimia 100.

 

Performance

Kichakata kazi cha Infinix ni Mediatek Helio Dimensity 8020 na Samsung ni Snapdragon. Snapdragon ni chipset hodari zaidi katika uchakataji kazi na ulizi pia.

Samsung ina Rom hadi kufikia GB512 na Ram ya GB8, Zero 30 Rom ni 256 na Ram 12GB na inaweza kuongezeka hadi kufikia GB 21 ya Ram. Ni rahisi kufungua file zaidi ya moja na kuzifanyia kazi kwa wakati mmoja pasipo simu kupata joto wala kustak kwa simu zote mbili isipokuwa zero 30 ni imara zaidi katika kipengele hiki.

 

HITIMISHO

Simu zote ni nzuri itategemea na budget yako kama inavyofahamika Samsung S23 ni gharama zaidi kuzidi Infinix Zero 30, kila kampuni na mbinu zake katika kuwafikia wateja nnavyofahamu Infinix Zero 30 ni kwajili ya kijana ambaye anatamani kuwa Vlogger.

 

Piga 0656317737 kwa huduma ya haraka.

9 Maoni

  1. issue the chipset tu ila Infinix ziko vizuri mno haswa battery ndio napenda zaidi.

    JibuFuta
  2. Simu iko vizuri na mimi ni mtumiaji wa Infinix kwa miaka mingi na battery yake iko vizuri nimeipenda sana ongezeko la vitu katika Ziro 30 jee hii inauzwa shingap na inanifikiaje Iringa Mafinga

    JibuFuta
    Majibu
    1. 0656317737 Wasiliana nao, Wanakutumia

      Futa
    2. Nimetumiwa ya kwangu, Naenjoy balaa. Hii simu nmeipiga chini juzi nkajua ndio mwisho wake. Lkn hata mkwaruzo hamna. Nmewakubali sana Infinix hii simu noma

      Futa

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi