TECNO NA MABADILIKO MAKUBWA YA SPARK 20 PRO+

 Simu ya kisasa utaifahamu kupitia muonekano wa nje, ufanisi wa camera namna inavyoweza kutoa picha kwa qualiti ya juu pamoja na ufanisi wa kichakata kazi au kwa lugha ya kiteknolojia tunasema Chipset. Hivyo vyote vinapatikana katika toleo la simu mpya mahiri SPARK 20 PRO+ ambayo ilizinduliwa sambamba na SPARK 20 pamoja na SPARK 20 PRO Decemba 2023.

Baada ya kukupa utangulizi wa nini kinavutia zaidi kwenye simu hii basi turudi kuichambua feature moja moja tukianza kuifungua.

TECNO SPARK 20 PRO+ ni simu yenye mwonekano mzuri sana na inakuja ikiwa katika sanduku lenye vifaa vya kutosha. Kuna kipochi, kilinda skrini ya glasi ambacho kimejipinda ili kufanana na onyesho la simu, vifaa vya masikioni vya USB-C, chaja ya 33W na kebo ya USB-A hadi USB-C.

Nyuma ina mfumo wa kamera wa mduara ambao umejengwa na camera kuu ya 108 na vihisi viwili vya msaidizi. Kwa upande mkali, kitengo cha 108MP kina kihisi cha inchi 1/1.67, kipenyo cha f/1.75 na zaidi inaongezeko la pikseli ‘9 in 1’ inanyakuwa mwangaza zaidi wa 900% kwa picha za usiku.

SPARK 20PRO+ ina onyesho la AMOLED, inawigo mpana wa kioo cha inch 6.78 na resolution ya 1080x2436px ambayo ni ya juu na ilaleta uhalisia wa rangi wakati wa kuangalia matukio mbalimbali ya picha na video kupitia simu yako na kimeongezwa ladha ya wepesi/smooth na referesh rate ya 120Hz kila unapoperuzi.

Helio G99 ndio imeipa ufanisi wa hali ya juu wa simu hii kuchakata games zenye ujazo mkubwa kama tumekubali ni gaming processor unafikiri ni nini SPARK 20 PRO+ itashindwa kufanya jibu ni hapana kwa simu za daraja lake SPARK 20 PRO+ ni moja ya simu ya kuifikiria kwa karibu katika chaguzi zako na zaidi simu hii inatumia mfumo mpya wa uendeshaji wa Android 14.

SPARK 20 PRO+ ina nafasi kubwa ya kuhifadhi kumbukumbu za mtumiaji, simu hii ya kisasa ina GB 256 Rom pamoja na Ram ya GB 16 inafanya mchakato mzima wa ufunguaji wa application au file zaidi ya moja kwa wakati mmoja kwa wepesi na kumpa mtumiaji uhuru kufurahiya nyakati za michezo, kujisomea n.k kwa wakati.

TECNO SPARK 20 PRO+ inapatikana katika maduka yote ya simu, fika katika duka lolote karibu nawe ufurahie teknolojia ya Camera ya ‘9 in 1’ kwenye simu hii yenye muundo wa Double Curved Design ikiwa katika rangi mbalimbali.

#TechLazima




2 Maoni

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi