Kuna Faida kutumia mitandao ya kijamii inaweza kuiletea biashara yako na kuweza kukusaidia kukuunganisha na wateja, kushirikisha, kukuza na kuimarisha biashara yako zaidi. Hizi ni baadhi;
1. KUKUZA UTAMBULISHO WA BIASHARA: Ikizingatiwa nusu ya idadi ya watu duniani ni watumiaji wa mitandao, kumbe basi matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii ni mbinu bora ya kuhakikisha biashara yako inajulikana zaidi duniani. Mfano tizama ilivyo ngumu kutangaza biashara mtaani katika kulipia gharama za matangazo ya televisheni na redio.
2. KUHUISHA BIASHARA: Siku hizi imekuwa ngumu sana kuamini bidhaa/huduma mpaka upate uthibitisho hai. Yaani uhakikishe hio biashara/kampuni ipo kweli na si matapeli. Hivyo, kupata wateja unatakiwa uonyeshe sehemu inayoishi (human side) ya biashara yako ambayo ni thamani ambayo biashara yako inaitoa kwa jamii. Mfano; hapa unaweza kueleza faida, umuhimu na namna za kutumia bidhaa/huduma yako. Elimu hii inapaswa iwe inatolewa mara kwa mara kupitia akaunti zako za mitandao ya kijamii. Mbinu hii hufanya biashara yako iweze kuishi katika maisha ya watu.
3. KUONGEZA TRAFFIC: Machapisho ya mitandaoni huchangia kwa kiasi kikubwa kuongeza traffic kwenye tovuti yako. Unaposhirikisha maudhui yaliyo kwenye tovuti kupitia machapisho unayoweka kwenye akaunti za mitandao unaiongezea thamani biashara kwenye shughuli za watu za kila siku kwa wao kuzidi kutembelea tovuti yako.
4. KUONGEZA WATEJA: Bila shaka dhumuni lako kubwa la kufanya biashara kupitia mitandao ya kijamii ni kuongeza wateja. Sasa mitandao hii inakupa njia nafuu zaidi ya kupata wateja wa bidhaa/huduma yako.
5. KUWASILIANA KWA UKARIBU: Ule msemo wa “Dunia ni kama kijiji” umefanya iwe rahisi zaidi kupitia matumizi ya mitandao ya kijamii. Yaani kupitia mitandao, sasa unao uwezo wa kuwasiliana kwa ukaribu na wateja wako kuhusu ubora wa bidhaa/huduma, kiwango, malipo n.k bila kujali umbali.
Hii imefanya iwe rahisi kutoa Huduma Bora kwa Wateja na kuimarisha uhusiano na ushirikishwaji wa wateja katika kuzalisha bidhaa bora na zenye viwango pamoja na kuhudumu kwa weledi wa hali ya juu zaidi.
#TechLazima
Chapisha Maoni