Mionzi ya simu za mkononi inaweza kuathiri maendeleo ya ubongo wa watoto walioko tumboni mwa mama zao, utafiti umeeleza.Utafiti huo umetaja madhara mengine ya mionzi ya simu za mkononi kuwa ni uharibifu wa manii, mimba, kupungua kwa nguvu za kiume, kupoteza kumbukumbu na kuzaa watoto watukutu.
Pia umeeleza kuwa matumizi kupita kiasi ya simu hizo, husababisha mtindio wa ubongo na upungufu wa udadisi kwa watoto tangu udogo wao.
Profesa Taylor ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Uzazi, Magonjwa ya Wanawake na Sayansi ya Uzazi, alisema: “Tulikuwa na panya wenye mimba katika maboksi na tuliwawekea simu juu ya vichwa vyao. Panya tuliokuwa tumewaweka katika bwawa lile, nusu yao walikuwa wazima na nusu yao walikufa. Panya waliokuwa hai tuliwaacha wajifungue na baada ya kujifungua, tukaanza kutafiti watoto wao.”
“Panya ambao hawakuwa karibu na simu za mikononi walionekana kuwa werevu. Kumbukumbu zao hazikupungua Utafiti huo umebaini kuwa kati ya asilimia tatu na saba ya watoto wenye umri wa kwenda
shule, wana tatizo la utukutu linaloweza pia kuathiri maendeleo yao kitaaluma.simu za mikononi pia ni sababu ya baadhi ya watoto kukosa adabu na pengine kutokuwa makini katika mambo mbalimbali wanapokuwa watu wazimaHuu ni utafiti wa kwanza unaoonyesha ushahidi wa madhara ya mionzi ya simu za mkononi. Tumeonyesha kuwa matatizo ya tabia katika panya yalitokana na mionzi ya simu za mkononi waliyoipata wakiwa tumboni,”Kuongezeka kwa utovu wa nidhamu kwa watoto kunaweza kuwa sehemu ya madhara ya mionzi ya simu, ambazo mama zao walikuwa wakizitumia wakati wao wakiwa bado tumboni.”
mionzi ya simu inaweza kusababisha kansa Matatizo yanayowapata watoto wa binadamu walio wengi hivi sasa ikiwa ni pamoja na magonjwa ya mtindio wa ubongo, mishipa ya fahamu inasababishwa na matumizi ya simu za mkononi kwa mama wajawazito pamoja na kukaa nazo jirani kwa muda mrefu.”
“Haijalishi mama anaongea na simu au la! Mionzi inapenya na kuleta madhara pia kusababisha kazi ya ukuaji wa mtoto katika ubongo kulegalega, wapo ambao wanalala na simu kitandani zikiwa zimewashwa... hii ni hatari zaidi labda iwe imezimwa.
#TechLazima
Chapisha Maoni