Sasa imekua rasmi diamond amemaliza mkataba na kampuni hii yasimu nchini Tanzania ambayo alikua amechukuliwa kwa mkataba wa mwaka mzima kwa africa mashariki.
Kampuni ya Itel ni moja mwa miongoni mwa kampuni za transsion ambazo ziko nchi za Africa, mnamo mwaka jana tar 04/04 kampuni hii yasimu ya itel iliingia mkataba na msanii nguli wa mziki ambaye ana tamba Africa na nchi za ugenini kwasasa na ku sign mkataba wa mwaka wa kutangaza simu zao upande wa digital kwani ndio sehemu ambayo watu wengi wanamtazama na kupeleka muziki wake duniani.
Msanii Diamond amekua akitumikia brand hii kwa muda wa mwaka sasa kimataifa haswa Africa mashariki kwa kutangaza kwenye mtandao wake wa kijamii zaidi ni instagram, diamond amefanikiwa pia kuhusisha familia yake kwenye kutangaza bidhaa za kampuni hii.
Taarifa kamili nikwamba diamond ameingia mkataba na itel na kuwapa familia yake kama bonus yaani nyongeza kwenye mkataba na pia kutumia vyanzo vyake vya ufikishaji wa habari yaani tv na redio kufikisha taarifa kwa kipindi cha mwanzo kilifanyika kwa nchi yote kujua rasmi kua sasa diamond amekua ni mwakilishi wa brand hii kwa Afrika mashariki.
Mkataba wake umeisha rasmi ila swali ambao lipo kwa waandishi wengi na wafuatiliaji wa trend na maendeleao ya kiteknolojia nikua.
- Je unadhani Diamond kuwa Brand Ambassador wa Itel
- Kumemshusha brand yake?
- kumemuongezea umaarufu?
- kumeongeza indosement?
- kumeongeza deal?
- au kumekuza uwekezaji wake.
- Je nini matokeo ya huu mkataba
- Diamond atapata deals nyingine?
- kufa kwa deals za simu kwa upande wake?
- Kuongezeka kwa wawekezaji wengine?
- Xiaomi
- samsung
- Huawei
- Infinix
- tecno
Chapisha Maoni