GARI MPYA YA MASUDI KIPANYA YA ZUA MZOZO



takribani ni miaka kwa miaka haijawahi kutokea kabisa kwa nchi ya africa mashariki Tanzania kua na ubunifu wa namna hii.

Mchoraji katuni wa Tanzania, Masoud Kipanya amezindua rasmi gari lake ambalo ni la kwanza la umeme kutengenezwa hapa nchini.

Kipanya, amesema gari hilo la umeme ni wazo lake binafsi la ubunifu ambalo lilimchukua miezi 11 kukamilika.

Gari hilo ambalo ni rafiki kwa mazingira kwa sababu halitumii nishati ya mafuta linaitwa Kaypee Motor na linachajiwa kwa saa sita kabla ya kutumika.

 "Hili ni gari la nguvu sana ambalo ukinunua unapata na chaji yake," alisema Kipanya wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika Hoteli ya Dar es Salaam Serena na kuhudhuriwa na baadhi ya wafanyabiashara nchini.

na gari hii imewekwa kwenye moja kati ya mall kubwa kabisa Tanzania ambayo ni MLimani city na mkurugenzi huyu amesema gari hii itakaa kwamuda kidogo hapo, na zaidi kwamba kwanzia sasa wanapokea order kwaajili ya wateja watakao hitaji gari hili.

Ukuaji wa teknolojia unazidi kupanuka kwa kasi sana na huu nimwanzo hivyo tunatarajia mambo makubwa sana siku za usoni kutoka kwa wataalamu wa Afrika na sasa tunajua na kuwakaribisha wawekezaji zaidi kwenye Teknolojia hii ambayo ameianzisha Masooud.

Endelea kutembelea kurasa zote za zoom teck kwa taarifa nyingi na za muda kuhusu teknolojia na updates zote.


#TeckLazima

Post a Comment

Mpya zaidi Nzee zaidi