Maendeleo ni moja kati ya sifa na chachu ya kuwa na mafanikio kwa nyanja mbalimbali, yaani ki binafsi, kifamilia, kiukoo, kiwilaya, kata , mkoa na hadi kinchi na kitaifa. kampuni za simu zimekua kiongeza kasi za maendeleo na uboreshwaji wa bidhaa zao kila siku kutokana na kasi ya kiteknolojia ya ulimwengu na hivyo kuipa sifa ya mafanikio nchi kadhaa zinapo peleka bidhaa zake.
kuna fununu ambazo si rasmi ila tayari zinasambaa na kwa baadhi ya nchi zisha achiwa huru juu ya kampuni ya simu INFINIX MOBILE kuja na simu Mpya aina ya INFINIX NOTE 12 VIP kampuni hii inaleta toleo hili la simu ya note 12, simu hii inakuja na maajabu mengi ambayo hayajawahi kufanyika kwenye matoleo ya nyuma kwa upande wa NOTE kutoka Infinix.
PROCESSOR/UCHAKATISHAJI
simu hii ya infinix Note 12 VIP inakuja na processor kubwa ya G96 hii kitaalamu inaitwa mediateck Helio G96 ambayo ni MT6781 na ni 12nm ukubwa wa uchakatuaji wa simu hii ni mkubwa kulinganishwa na simu nyingine ambazo zishawahi kutokea huko nyuma na hivyo kuleta namna ya utofauti ndani ya simu hii ambayo inaupa uwezo mkubwa wa ufanisi wa simu, kwa wale wapenzi wa kucheza game simuu hii ina wafaa sana na wale wapenzi wa movie ina wafaa pia zaidi kwa wale watumiaji wa simu kiofisi zaidi yaani document zaina tofauti ma file makubwa yote unaweza kufungua kwa wakati mmoja na bila simu yako ku stuck muda unatumia.
REFRESH RATE/ UNG'AMUZI
ujio huu wa simu hii unatarajiwa kuwa watofauti kwani simu hii itakuja na kioo chenye uang'avu wa ajabu na zaidi kina kiwango cha kuonyesha upya chenye kasi zaidi yaani refresh rate yake ni 120hz hii iko fasta na chap kwenye simu hii, fahamu zaidi juu ya refresh rate GUSA HAPA na si refreshrate tuu bali kioo chake kina picha halisia yaani Amoled desplay kinakupa uwezo wakuona vitu kwa quality ya juu zaidi tofauti na ukitazama kwenye simu nyingine. pia unaweza kusoma na kuelewa zaidi juu ya Amoled display HAPA.
CAMERA/KAMERA
Infinix Note 12 VIP inakuja na camera ya 108mp, hii ni camera ya juu zaidi hakika itawapa nafasi watumiaji wa simu haswa kwa wale wanao penda picha zaidi kufurahia simu na matumizi ya simu yao kwa utumiaji wa simu hii kwani ina mfururizo wa jabu kutokea kwa matoleo ya Note kwa kampuni ya Infinix, haikuwa rahisi kwa kampuni hii japo ilisha toa aiana au kameara yenye uwezo wa juu hivi hapo nyuma kwa toleo la Zero na yo ilikua ni zero X pro ila imeongeza chache na matumizi makubwa ya kamera kwa toleo hili. inasemekana simu hii itakua na Wide ambayo ni 108 MP, f/1.8, (wide), 1/1.67", 0.64µm, PDAF, Laser AF pia na Ultra wide yenye 13mm f/2.2 na depth ambayo iko na 2 MP, f/2.4 na uwezo wa video ni 1440p@30fps, 1080p@60fps.
BATTERY/BETRI
Infinix imekua ikisifiwa na inaongoza kwa kutoa matoleo yanayo kaa na chaji zaidi kuliko simu nyingine, hii inatokana na sifa za kila toleo hivyo tetesi zinavuma kua Simu hii Note 12VIP kutoka infinix inakuja na bettry 4500mAh ila hii sio kubwa kinacho shangaza ambacho hata zoom tech pia tunasubiri kujaribu simu hii kutokana na uvumi huu ni kasi ya kuchaji simu hii inachukua dakika 17 tu kwa Note 12 VIP iliyo zima chaji kabisa kuijaza kufika 100% ndani ya dk17, kwa rugha nyepesi simu hii ni fast charge na nizaidi ya balaa kwenye soko la simu pamoja inakuja na watts 120w.
PRICE/BEI
Hata na baada ya kuwa na vitu vyote hivyo bado simu hii inasemekana ni economy yaani nikwaajili ya watanzania na waafrika hivyo haitakua na bei kubwa hivyo kama invyo vuma huko kwenye baadhi ya kurasa za wachambuzi wengine, taarifa hizi zimetufikia Zoomtech na kwasababu hiyo tuna wahakikishia watanzania na wote kua simu hii inasemekana haitakua na bei ya kutisha kuto kununua yaani nikwaajili ya watu wote na hapa ndipo walipo jitahidi kampuni hii ya simu kwani imeweza kushika soko la Afrika na hivyo basi ni nafasi ya kila mtanzania ku furahia ulimwengu wa teknolojia ndani ya simu mpya kutoka infinix itakayo kuja siku chahce zijazo INFINIX NOTE 12 VIP.
endelea kufuatilia kurasa zetu za zoomtech kwa updates za kila siku juu ya teknolojia.
#TECHLAZIMA

Safi sanaaa
JibuFutaSafi sana
JibuFutaKweli hizi simu ni nzuri maana hata ninayo tumia inakaa chaji
JibuFutaOk
JibuFutaChapisha Maoni