Infinix NOTE 12G88 Yapata matokeo mazuri kulinganisha na Samsung A22

 Karibu tena kwenye ukurasa wetu, Leo tutaangazia kwa kina sababu ya kwanini simu ya kampuni inayokuja kwa kasi sana ya Infinix Mobility, Infinix NOTE 12 G88 kutoka kwenye Series ya NOTE 12  inapata matokeo mazuri zaidi kuliko simu ya kampuni ya Samsung, Samsung A22.



Tupitie Specs zake na bei kwa pamoja ili tujue kwanini Infinix NOTE 12 G88 inakuja mbele ya Samsung A22;

Display; Infinix NOTE 12 G88 ni AMOLED inch 6.7 = Samsung A22 ni AMOLED

Simu hizi zote mbili zina AMOLED display lakini ukiingia kwa undani zaidi kwenye display Infinix NOTE 12 G88 ina 1080x2400 Pixels huku Samsung A22 ikiwa na 720x1600 Pixels.

Kwa maana hii ni kuwa pamoja na zote kuwa Amoled ila bado simu ya Infinix NOTE 12 G88 itakuwa na onesho zuri zaidi kwa maana ina uwezo mkubwa zaidi.


Camera; Infinix NOTE 12 G88 ina 50MP  = Samsung A22 ina 48MP.

Kwa upande wa kamera simu ya Infinix NOTE 12 G88 ina uwezo mkubwa zaidi ya Samsung A22 ambayo imezidiwa kwa Mega Pixels ikiwa NOTE 12 G88 ina 50 MP, f/1.6, (wide), 1/2.8", 0.64µm, PDAF, 2 MP, f/2.4, (depth), QVGA huku Samsung A22 na 48MP camera.

Hapa pia Infinix Ikiwa imeongoza tena.


Battery; Infinix NOTE 12 G88 ina 33W Fast Charging  =  Samsung A22 ina 15W Fast Charging

Kwa sasa Infinix wanasifika kwa kuwa watangulizi kwennye teknolojia ya Fast charging kwa maana kuna rumors kuwa wataweza kutoa simu yenye teknolojia ya kuweza kuchaji simu ndani ya dakika 10 ikiwa imeongeza kutoka  kwenye simu mwenza NOTE 12 VIP ambayo inachaji ndani ya dakika 17.

Infinix NOTE 12 G88 ina 33W Fast charging  ikiipita mbali simu ya Samsung A22 ambayo inajikongoja na 15W Fast Charging.

Hiyo ni hatua nyingine Infinix NOTE 12 G88 ikitangulia tena.


Processor; Infinix NOTE 12 G88 ina MediaTek Helio G88 = Samsung A22 ina MediaTek Helio G80

Kwa upande wa utendaji kazi wa simu hizi mbili Infinix NOTE G88 inaonesha wazi kuwa na uwezo mkubwa zaidi kwa maana imeipita kwa kuwa na MediaTek Helio G88 huku Samsung ikiwa na Processor ndogo yenye MediaTek Helio G80.

Mpaka hapa Infinix NOTE 12 G88 Imechukua point nne mbele Samsung A22.


Upatikanaji;

Infinix NOTE 12 G88 inapatikana kwa Tsh. 480,000/= na kama ilivyo tangazwa kupitia mitandao ya kijamii ya @infinixmobiletz bado wanaendelea na promosheni na ukinunua simu hii unapata nafasi ya kushinda TV, LapTop, Shoping Voucher, Piki Piki na Dstv Sett au NOTE 12 VIP mpya. 

Samsung A22 inapatikana kwa Tsh. 500,000/=.

Kwa mahitaji na mawasiliano ya haraka Tupigie kwa namba hii 0743558994, Pia usiache kutufuatilia kwenye mitandao ya kijamii kwa jina la ZOOM TECH kwa taarifa zaidi za teknolojia kwa lugha hadhimu ya Kiswahili.


#TechLazima

19 Maoni

  1. Sawa mmesomeka

    JibuFuta
  2. Hyo note 88 inauzwa shingapi

    JibuFuta
    Majibu
    1. Nata bei ya hyo simu na inauzwa wpi

      Futa
  3. Cm zenu ni nzuri sawa na mnazitangaza asa mbn upatikanaji wake ni mgum mikoan

    JibuFuta
  4. Mko vizuri!

    JibuFuta
  5. Simu zenu ninzuli Ila hazishuki bei

    JibuFuta
  6. Shingap hiyooo no mzuri

    JibuFuta
  7. Nahitaji hiyo cm ntaipataje?

    JibuFuta
  8. Mko powa Bei vip

    JibuFuta
  9. Kwani tecno comon 19 ni shingapi ?na Infinix note 12 gb 64 ni shingapi?

    JibuFuta
  10. Mm nataka iyo sim

    JibuFuta
  11. Nzuri sana,naitaka

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi