Baada ya Infinix HOT 12, Kampuni ya simu Infinix inaashiria
ujio wa muendelezo wa series ya HOT. Simu hiyo inayosemekana kuwa ni HOT 30 kwa
mujibu wa taarifa mbalimbali zinazotupiwa na mtandao wa kijamii wa kampuni ya @infinixmobiletz ni dhahiri simu hiyo iliyoundwa vyema na camera ya
MP50 kuzinduliwa Mwezi huu wa April.
Mabadiliko kwenye HOT series si
kwa camera tu Infinix imefanya mabadiliko makubwa mno katika kila kipengele.
Tukianza na swala la chaji, Infinix HOT 30 kuja na Wat33 na battery la mAh si
chini ya 5000 inasemekana HOT 30 hujaa chaji kwa haraka zaidi inachukua dakika
30 tu kufikia 100%.
Pia inasemekana Infinix HOT 30 ni
simu yenye muonekano wa kuvutia kuwahi kuwepo ni simu ambayo kijana yoyote
atatokea kuipenda na kimuonekano ni nyembamba sana na huenda ikawa ni nyepesi
na kuweza kuihifadhi hata kwenye mfuko wa shati. Muundo wa juu ni kama kioo
pande zote yani kama inch 6.78 moja ya picha ambazo zinaonekana kupigwa na HOT
30 inaashiria resolution ya kioo cha simu hii huenda ni zaidi ya 1080P.
Kuhusu bei bado
haijafahamika lakini kwa nyepesi nyepesi zilizopo simu hii huenda ikawa bei
sawa na HOT 12 au chini zaidi, HOT 30 si simu ya kukosa kaa karibu na @infinixmobiletz.


Hii ishaingia sokoni??? Ukiacha Ile nyingine Ndogo niliikuta sasa nataka Hii jamani ile Ndogo hapana naomba Nijulishe ikifika
JibuFutaIpo Bei ni 450,000/=
FutaMbadilishe na system za ndan muundo wa apps zote n ule ule,SA ndo NN?Kwa nje inaweza kua nzur lkn ndan Mambo n yaleyale!Mnaboa bhana
JibuFutaNmeipenda
JibuFutaChapisha Maoni