BAADA YA HOT 12 NA MEDIATEK HELIO G85, 13MP SASA NI HOT 30 NA MEDIATEK HELIO G88 NA 50MP CAMERA.

 

Baada ya Infinix HOT 12, Kampuni ya simu Infinix inaashiria ujio wa muendelezo wa series ya HOT. Simu hiyo inayosemekana kuwa ni HOT 30 kwa mujibu wa taarifa mbalimbali zinazotupiwa na mtandao wa kijamii wa kampuni ya @infinixmobiletz ni dhahiri simu hiyo iliyoundwa vyema na camera ya MP50 kuzinduliwa Mwezi huu wa April.



Mabadiliko kwenye HOT series si kwa camera tu Infinix imefanya mabadiliko makubwa mno katika kila kipengele. Tukianza na swala la chaji, Infinix HOT 30 kuja na Wat33 na battery la mAh si chini ya 5000 inasemekana HOT 30 hujaa chaji kwa haraka zaidi inachukua dakika 30 tu kufikia 100%.


Pia inasemekana Infinix HOT 30 ni simu yenye muonekano wa kuvutia kuwahi kuwepo ni simu ambayo kijana yoyote atatokea kuipenda na kimuonekano ni nyembamba sana na huenda ikawa ni nyepesi na kuweza kuihifadhi hata kwenye mfuko wa shati. Muundo wa juu ni kama kioo pande zote yani kama inch 6.78 moja ya picha ambazo zinaonekana kupigwa na HOT 30 inaashiria resolution ya kioo cha simu hii huenda ni zaidi ya 1080P.

Kuhusu bei bado haijafahamika lakini kwa nyepesi nyepesi zilizopo simu hii huenda ikawa bei sawa na HOT 12 au chini zaidi, HOT 30 si simu ya kukosa kaa karibu na @infinixmobiletz.

#TechLazima

4 Maoni

  1. Hii ishaingia sokoni??? Ukiacha Ile nyingine Ndogo niliikuta sasa nataka Hii jamani ile Ndogo hapana naomba Nijulishe ikifika

    JibuFuta
  2. Mbadilishe na system za ndan muundo wa apps zote n ule ule,SA ndo NN?Kwa nje inaweza kua nzur lkn ndan Mambo n yaleyale!Mnaboa bhana

    JibuFuta
  3. Nmeipenda

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi