Kampuni ya Simu janja ya Infinix Mobile Tanzania imeendelea na dhamira yake ya kunyanyua vijana kupitia vipaji vyao na kuwapa nafasi ya kuonesha uwezo wao ili wapate kutimiza ndoto zao.
Tarehe 13/06/2023 Infinix kupitia ukurasa wao Instagram @infinixmobiletz walitangaza programu ya Star Alliance (#SpidiKasi Challenge) inayowapa vijana weye vipaji vya kuimba, kuchana (rappers) na Dancers nafasi ya kuonesha vipaji vyao na kuahidi zawadi nono kama record deal, promotion mwezi mzima, performance na msanii wa kizazi kipa Marioo kwenye Fainali za challenge hii zinazotegemewa kufanyika tarehe 12/08/2023 Warehouse Masaki.
Kwa sasa programu hii ya Star Alliance ipo kwenye hatua ya mwisho ambapo wametangazwa kumi bora kwa upande wa waimbaji/Rappers na upande wa Dancers
Na sasa mchakato wa kupiga kura unaendelea, Kwa mujibu wa @infinixmobiletz mwisho wa kupiga kura itakuwa tarehe 08/08/2023.
Hapa jinsi ya kumpigia kura mshiriki wako pendwa;
1. Tembelea ukurasa wa instagram @infinixmobiletz
2. Fungua Link kwenye Bio ya @infinixmobiletz au Fungua Link hii >> https://linktr.ee/Spidikasi.Top10.Vote
3. Fungua kila kipengere na Mpigie mshiriki wako bora ili apate kushinda.
Pia unaweza kushinda Tiketi ya bure kuhudhuria Tamasha la Fainali hizi kwa kujibu swali kwenye ukurasa wa @infinixmobiletz (Kwanini unadhani unastahili kupewa Tiketi Bure?)
Она
JibuFutaChapisha Maoni