Kampuni ya simu za mkononi Infinix yenye matawi yake barani Africa, Asia na Laten America imeshangaza wengi kutokana na hatua kubwa ya kushirikiana na Kampuni ya Mbio za Magari BMW kuleta ubunifu kwa matoleo mapya ya Note 30 Vip.
Taarifa ya @infinixmobiletz @infinixglobal wakati wa kuunda NOTE 30 VIP, tulishirikiana na BMW Design Works ili kuboresha mwonekano na kuwa yenye kuendana na urembo unaowakilisha kasi ya utendaji kazi wa hali ya juu zaidi”.
BMW tunaifahamu kama Brand imara yenye bidhaa zenye ubunifu mzuri wa mwonekano, speed kwenye vyombo vyake vya moto lakini pia tunaifahamu Infinix kama brand ya vijana wenye kupenda tech, fashion na mitindo ya kisasa na kupitia matoleo yake mbalimbali hasa hili la NOTE Design na Speed imekuwa kipaombele kikubwa.
Mbali ya kuwa na mwonekano wa vyombo vya moto vya BMW lakini pia simu hii sifa yake kubwa ni ufanisi wa hali ya juu. Note 30 vip ilitangazwa kuwa simu yenye teknolojia ya kisasa ya fast chaji ambayo inagharama nafuu ya bei kulinganisha na simu za makampuni mengine zenye sifa sawa na hii.
Fast chaji ya NOTE 30 Vip ina Watt 68 na Wireless chaji ina Watt 50 lakini pia simu hii inauwezo wa kureverse chaji kwa simu nyengine.
Simu hii mahiri napendekezo sahihi kwa vijana inaongozwa na Android 13 lakini pia inachakataza kazi kwa kutumia process Mediatek Dimensity 8050 ikisaidiana na Ram yenye kuongezeka hadi kufikia 21 na kufanya mtumiaji kuweza kufungua files nyingi na kuzifanyia kazi kwa wakati mmoja pasipo kugoma au kupata joto.
Uwezo wa camera wa simu hii ni advanced, simu hii inacamera 3 nyuma na kamera kuu ni megapixel 108 lakini pia inauwezo mzuri wa kurecord video wa mfumo wa 4k na kukupa picha halisi ya tukio zima ikifanya kazi sambamba na AMOLED Display yenye refresh rate ya 120Hz.
Kwa hakika Design na Speed imezingatiwa kwa hatua kubwa katika simu hii na pamoja ya kuwa ni toleo jipya lakini tayari NOTE 30 Vip BMW imeramba tuzo ya iF Design Awards 2023.
Tunakaribisha maoni hapo chini lakini pia unaweza wapata kupitia namba 0656317737.
Bravo wakat umefika na sisi watumiaji wa lnfinix kutamba
JibuFutaIvi hiyo simu inauzwa shingapi
Futaaround $363
FutaInfinix forever
JibuFutaHiyo inauzwa km laki tisa na kitu
FutaHi g
FutaSaddamali250
JibuFutaلدي نوت 30 vip يستهلك Ø´ØÙ† كثيرا ما المشكلة
JibuFutaChapisha Maoni