Kampuni ya simu za mkononi Infinix Mobile yenye makao makuu yake jijini Hong Kong ikishirikiana na kampuni ya Ma game Garena kufanya ghafla ya uzinduzi wa matoleo ya HOT 40 nchini Tanzania utakao sindikizwa na mashindano ya Game la FREE FIRE.
Tovuti mbalimbali za tech ikiwemo @infinixmobiletz imetupia picha mbalimbali zenye jumbe zinazoashiria ufanisi mkubwa wa matoleo ya simu za HOT 40 katika uchakataji pamoja na upelekaji/ ujazaji chaji kwa haraka zikiweza kufanya hayo kwa maboresho makubwa yaliyofanyika kwenye processor aina ya Mediatek Helio G99 ikiwekewa XBOOST gaming Engine pamoja na fast charging watt 33 yenye kujaza chajaza chaji kwa dakika 5 na kuruhusu matumizi kwa masaa 2.
Infinix imeandaa uzinduzi wa HOT 40 kwa mfumo huu ili kujumuika na vijana wote kushuhudia maboresho hayo makubwa yaliyofanyika katika series hii lakini pia kuleta ile chachu ya FAST and FUN kwa vijana kupitia bidhaa zao. Dirisha la kujisajili lipo wazi kuanzia sasa kupitia BIO @infinixmobiletz https://forms.gle/xGoaRVZ6Najt7Dtq8 ambapo mashindano yatafanyika kwa siku mbili Decemba 15 na Decemba 16 katika viwanja vya Mlimani City na washindi kuondoka na HOT 40pro kwa kila mmoja na kitita cha Tsh.1,000,000.
Chapisha Maoni