TUIFAHAMU INFINIX HOT 40 PRO SIMU ILIYOGUSA KWA UKARIBU VIJANA NA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU 2023/2024.

 Kampuni ya simu za mkononi Infinix Mobile Tanzania iliumaliza mwaka 2023 kwa mafanikio makubwa yaliyoletwa na matoleo ya simu mpya katika mwaka huo, kama ilivyo lengo la kila kampuni kufikia wateja wake kwa wingi hasa katika kipindi cha uwepo na bidhaa mpya sokoni Infinix ilifanikiwa kufanya hivyo kwa asilimia kubwa kupitia simu yake mpya ya Infinix HOT 40 pro.

Muonekano wa Infinx HOT 40 Pro ikiwa katika rangi mbalimbali.

HOT 40 pro ikiwa ni simu ya funga Mwaka na kuanzia Mwaka, Kampuni hii yenye jopo kubwa la wateja ambao ni vijana imeitengeneza simu hii kwa features zenye kuwapendeza vijana, miongoni mwa features hizo ni Chipset ya Helio G99 ambayo inaufanisi mzuri katika uchakati ikiwemo uchezaji wa mobile gaming ambapo pia simu hii ina Engine ya XBOOST pamoja na sensor ya Gyroscope kwajili ya kufanya balancing katika uchezaji wa mobile game.

FREE FIRE na Tigo Tanzania partners wa Infinix HOT 40 pro.


Sifa kuu nyengine ni fast chaji ya watt 33 ambayo endapo simu inaasilimia 20 ya chaji basi kwa kutumia dakika 35 tu simu yako itakuwa imefikia zaidi ya asilimia 75 ya chaji, Infinix pia imehakikisha swala la kamera ni muhimu HOT 40 pro inamegapixel 108 nyuma na megapixel 32 ambazo zinateknolojia ya kisasa ya kuchukua matukio kwa kamera zote mbili kwa wakati mmoja.

Gamers walivyojumuika kushiriki FREE FIRE mobile game.

Ni vipi Infinix iliweza kuwafikia wengi katika kipindi kifupi? HOT 40 pro ilizinduliwa kiana yake katika Mall ya Mlimani City jijini Dar es Salaam. Infinix ilialika vijana kuhudhuria zinduzi huo pasipo kiingilio ambao ulifanyika sambamba na mashindano ya mobile game vijana walichuana kwa mchezo wa FREE FIRE ambapo washindi walizawadiwa kiasi cha shilling 1,000,000 pamoja na simu za Infinix HOT 40 pro kwa kila mwanakikundi.

Washindi wa FREE FIRE Mobile game.

Haikuishia hapo Infinix iliamia kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwa kusogeza huduma za Infinix vyuoni na kuwapa nafasi pia yakuonyesha vipaji vyao kupitia challenge iliyofahamika kama #kubwayamoto ambayo ilikuwa ikifanyika kupitia mtandao wa kijamii wa tiktok @infinixmobiletz

Wanafunzi wa elimu ya juu wakipata maelezo kuhusu Infinix HOT 40 Pro.

Washiriki waliongia kumi bora walizawadiwa gift package ambayo ilikuwa na bag, watter bottle pamoja na zawadi nyengine za brand ya Infinix lakini pia mshindi wa kwanza alizawadiwa Infinix HOT 40 pro.

Washindi wa kubwa ya moto challenge.

Infinix pia iliwagusa wateja wake ambao walifanya manunuzi katika maduka yao ya simu kwa kipindi hicho cha Mwezi Desemba kupitia promosheni ya #KubwayaMoto kila mteja aliyefanya manunuzi katika kipindi hicho hakuondoka kinyonge, mbali na zawadi za papo hapo pia walitoa zawadi ya Scooter, Laptop 6 na simu 12 kwa wateja walioshinda droo kubwa la bahati nasibu.

Mshindi wa Scooter katika promosheni ya Kubwa Ya Moto.

Hii ni njia moja wapo ambayo kampuni hii iliitumia kuonyesha upendo kwa wateja wote wakati wa kuikaribisha simu ya Infinix HOT 40 Pro nchini Tanzania. Simu hizi na nyengine nyingi zipo madukani unaweza lipa kidogo kidogo ‘Mkopo’ au kiasi chote kwa wakati mmoja. Tembelea duka lolote la simu kupata bidhaa zao au tembelea @infinixmobiletz


##TechLazima



5 Maoni

  1. I love how lnfinix connect with customer great

    JibuFuta
  2. Hakika Infinix imetusogeza karibu na Dunia

    JibuFuta
  3. Wametisha sana

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi