Fahamu njia rahisi za Kupunguza matumizi ya Internet kwenye simu yako

 

Leo tunaendelea na sehemu ya pili ya namna ya kupunguza matumizi ya internet (bando) kwenye simu yako...

...YouTube haina tofauti sana. Unaweza kutumia hadi MB 260 kwa saa kuangalia video yenye ubora wa 480p, wakati video yenye ubora wa kiwango cha juu (HD: 720p na 1080p) inaweza kukugharimu hadi GB 1.65 kwa saa. Video ya 4K huweza kutafuna hadi GB 2.7 za data kwa saa.

Si video tu, hata kiwango cha matumizi ya data kwa kusikiliza muziki mtandaoni kinatofautiana kutokana na kiwango cha ubora wa sauti utakachokichagua. Baadhi ya majukwaa ya muziki mtandaoni kama vile Apple Music na Spotify yanakupa uhuru wa kuchagua kiwango cha ubora, kama vile Low, Normal na High. Kwa kiwango cha Low, unaweza kutumia wastani wa MB 43 kwa saa, Normal inaweza kufika hadi MB 72 kwa saa na kwa kiwango cha High inaweza kufika MB 115 kwa saa.
Viwango vyote hivi ni makadirio ya wastani, na huweza kubadilika kutokana na kiwango cha ubora wa upatikanaji wa mtandao wa intaneti unaoutumia.

Njia rahisi ya kuangalia video au kusikiliza muziki mtandaoni bila kukunja nafsi kwa wasiwasi wa kuishiwa bando ni kupunguza kiwango cha ubora wa video au muziki. Ingawa unaweza kukosa ubora unaoutaka, utakuwa na uhakika wa kuendelea kutazama au kusikiliza kwa muda mrefu zaidi.

Unawezaje kufahamu kiwango cha data unachokitumia mtandaoni?
Pengine ungependa kufuatilia matumizi yako mtandaoni kwa sababu tofauti, ikiwamo kujiwekea ukomo wa kiwango cha matumizi. Teknolojia inakuruhusu kufanya hivyo.
Kwa watumiaji wa iPhone, nenda kwenye Settings > Mobile > Mobile Data Usage. Hapo utaweza kuona kiwango cha matumizi yako ya data.
Na kwa watumiaji wa Android, fungua "Settings" kisha fungua "Data Usage" chini ya "Network & Internet."

kama bado haujafahamu ama umeshindwa kutatua changamoto hii tafadhali toa maoni yako hapo chini kwa msaada zaidi.

#TechLazima

2 Maoni

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi