Infinix NOTE 11 Pro Ni tishio kwa Samsung A32



Maajabu kwenye ulimwengu wa teknolojia,

kampuni ya simu ya Infinix Mobile imefanikiwa kuukimbiza mwenge na kuwa bora zaidi kwenye toleo lake la hivi karibuni na kuwapa kigugumizi kampuni ya samsung mobile,

Ni dhahiri kua kampuni hii ya samsung imekua ikiwa na mabavu na watumiaji yaani wateja wake wamekua wakiamini zaidi lakini kampuni ya simu za infinix imekuja na toleo lake la NOTE na kuipa changamoto na kushusha mauzo ya toleo la A kwa samsung. 

Infinix NOTE 11 Pro imeua soko na kusimamisha mauzo ya Samsung A32 kwa kuja na specification zake ambazo ni bora zaidi kwa watumiaji wasimu ukilinganisha na toleo la Samsung A32.

Tazama Umaridadi wa Infinix Note 11 pro ukilinganisha na Samsung A32.

  • PROCESSOR 
mfumo wa uendeshaji wa Toleo jipya la Infinix Note 11 pro ni mkubwa zaidi kuringanisha na Samsung A32, yaani kwa upande mwingine Note 11 Pro imeweza kurahisisha matumizi ya simu na kazi kwa ujumla kwa wateja wake kwani unaweza kutembea na simu yako kama office yako na kampuni hii inakuhakikishia kua Note 11 pro inaweza kufanya kitu ambacho kompyuta inaweza kufanya kwasababu ya processor yake ambayo ni G96 na refresh rate ya 120hz  ni processor yakwanza kwa simu za android kuingia Tanzania ukilinganisha na processor ya Samsung A32 ni G80 na refresh rate ya 90hz ni processor ambayo teali makampuni mengine yanayo na pia processor ambayo ilishazoeleka, kwa wapenzi wa game muvie na vinginevyo Infinix note 11 pro unaweza kufanya vyote kwa pamoja. kufahamu zaidi juu ya ubora na matumizi ya refresh rate Gusa HAPA kufahamu zaidi umuhimu wa refresh rate kubwa ambayo inayo Note 11 pro kutoka infinix 120Hz

  • BATTERY
Suluhisho la kutunza chaji na kuokoa pia muda wa mtumiaji kampuni ya infinix imeweza kutatua tatizo hili ambalo liko kwa watumiaji wengi wa simu janja za mkonono na hivyo toleo jipya la Note 11 pro in betri ya 5000mAh huku ikiwa na 33W ambayo ni fast chaji yaani unajaza simu yako kwa muda mfupi na kuendelea na matumizi ukilinganisha na Samsung A32 ina 5000mAh na 15W ambayo ni ndogo kwa 33W, kwa mtumiaji wa A32 atasubiri kidogo kwa muda wakati mtumiaji wa Note 11 pro atakua ameshajaza chaji simu yake lisaa limoja nyuma ya A32. 


  • CAMERA
kufuatana na camera zinalaingana ila bado kuna mwanya katikati ya haya matoleo mawili kwani Note 11 pro ina 64MP na inauwezo wa ku zoom hadi 30X kitu ambacho A32 hakina kwenye kamera na kubakiza tu 64MP, kulingana na matumizi ya simu ya watu siku izi ya ku zoom in na ku zoom out Note 11 pro imeiacha mbali sana toleo la Samsung A32 kwnye kamera.


  • STORAGE
ukubwa wa memory ni sababu kubwa inayo fanya watu wazidi kutumia na kutamani kununua simu hii Note 11 pro  ambayo ina Ram ya 8GB na storage ya 128GB kulinganisha na A32 ambayo bado imejigawanya sana kwani wametoa matoleo tofauti tofauti kwa upande wa storage wana storage ya 4GB, 6GB na 8GB kwa simu moja hii inaonesha hali ya kuto kujiamini na kutoa storage moja na kuigawanya mara tatu,

  • BEI
Infinix Note 11 pro ukiacha kua na sifa zote hizo bado bei yake ni yawatu wote yaani kila mtanzania anaweza kununua iwe kwa kujidunduliza hata kwa mkupuo lakini uhakika wakila mtanzania kuimudu. Infinix Note 11 Pro inapatikana madukani kwa bei ya 650,000 tsh tuu, kulinganisha na A32 ambayo bei yake sio chini ya 700,000 na kuendelea.

  • UPATIKANAJI
Infinix Note 11 pro inapatikana madukani kote Inchini Tanzania ncje na ndani mwa Dar es salaam yaani mikoa yote unaweza kupata Infinix Note 11 pro na kwasasa wana offa ambapo ukinunua simu hii unaweza kujishindia zawadi kem kem.

Tembelea page za infinix mobile Tz na kurasa zao zote kupata Updates za kila siku, pia usiache kutembelea Zoomtech kwa updates za kila leo na kila saa.

TechLazima

16 Maoni

  1. Mnazingua Mm natumia Samsung na siwezi jaribu hiyo Infinix

    JibuFuta
    Majibu
    1. Wanazingua na nini we sema sio mpenzi basi

      Futa
  2. Naikubari sana Infinix

    JibuFuta
  3. Tuko pamoja infinix

    JibuFuta
  4. Dahhh hizi chuma zinakaa na chaji kinoma hatari Sana..

    JibuFuta
  5. Uzuri wa infinix kwenye chaji mmepita

    JibuFuta
  6. Nakubali sana hiyo ndio yenyewe sasa nilikuwa na lengo la kununua Infinix NOTE 10. nimeailisha lazima ninunue hiyo NOTE 11

    JibuFuta
  7. Nimeikubali, nazipenda Infinix kwa kutunza charge bwana.

    JibuFuta
  8. Infinix ndo mkombozi wangu simu nzuri bei nzuri 💪👏🙏

    JibuFuta
  9. Hakuna ubishi Tanga infinix zimeingia tz tatizo la chage tulishasahau, chage inakata kwa muda mrefu

    JibuFuta
  10. Sina ulimwengu mwingine Zaid ya Infinix nawakubar

    JibuFuta
  11. 𝐼𝑛𝑓𝑖𝑛𝑖𝑥 𝑘𝑤𝑒𝑛𝑦𝑒 𝑐ℎ𝑎𝑗𝑖 𝑖𝑘𝑜 𝑝𝑜𝑎 𝑠𝑎𝑛𝑎𝑎𝑎𝑎𝑎𝑎𝑎𝑎

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi