SAMSUNG YASALIMU AMRI KWA KAMPUNI YA SIMU INFINIX

 


Leo tutaangaza ni namna gani Kampuni ya simu Infinix imeweza kuwa tishio kwa makampuni kongwe kama Samsung na nyenginezo kwa kulinganisha bidhaa ambazo zimeingia sokoni mwaka huu na zimekuwa zikifanya vizuri “Infinix NOTE 12 na Samsung Galaxy A23”.



Vipengele ambazo tutaviangazia ni Ukubwa wa memory, qualiti ya kamera, utunzaji chaji na ujazaji chaji kwa haraka, CPU kasi ya processor na ubora wa aina ya display.

TOFAUTI Infinix NOTE 12 V/S Samsung Galaxy A23.

Ø  Dislpay - Infinix NOTE 12 ni AMOLED inch6.7 / Galaxy A23 ni PLS LCD inch 6.6.

 

Infinix NOTE 12 na Galaxy A23 zinawigo mzuri wa kioo unaweza angaza matukio mbalimbali kupitia simu yako kwa nafasi ya kutosha isipokuwa kwenye aina ya kioo AMOLED ndio kioo bora kwa sasa sababu kinautajiri wa rangi hivyo picha ama video huonekana kwa qualiti ya hali ya juu kulinganisha na kioo cha PLS LCD kilichopo kwenye simu hii ya Samsung A23 lakini vile vile AMOLED inasaidia uwasilishaji wa taarifa kwenye CPU kufika kwa haraka zaidi hii husaidia pia mfumo wa utumizi wa chaji kwa mdogo.

 

Ø  Memory Storage – Infinix NOTE 12 ni 128Rom + (8Ram+5Ram) / Galaxy A23 ni 128Rom + 6Ram.

Simu hizi mbili zinashabihiana upande wa ROM isipokuwa zinatofauti ukubwa ya RAM. Rom ni chumba cha kuhifadhia kumbukumbu na RAM huipa program/application ni mahali pakuhifadhi na kufikia taarifa kwa muda mfupi ili simu iweze kufanya mfumo wa uendeshaji mawasiliano kuwa wa haraka, kwa mujibu wa uwezo wa Ram wa simu hizi mbili Infinix NOTE 12 inauwezo mkubwa kwa kuhifadhi taarifa nyingi zaidi ukilinganisha na Galaxy A23 na hii inafanya hatari ya kustuck kwa simu ya Samsung Galaxy A23 kuwa kubwa.

Ø  Fast Charging Watt- Infinix NOTE 12 ni 33Watt / Galaxy A23 ni 25Watt.

Simu hizi mbili zinaujazo sawa wa battery zote zikiwa na mAh5000 isipokuwa tofauti ipo kwenye teknolojia iliyotumika kuchaji simu NOTE 12 ina watt 33 inakuchukua lisa limoja kasoro kujaa asilimia 100% na Galaxy inakuchukua lisaa na zaidi kujaa asilimia 100%. Muda ni muhimu sana zingatia unapofanya maamuzi ya kununua simu.

Ø  Camera – Infinix NOTE 12 selfie 16Mp / Galaxy A23 selfie 8Mp.

Kamera ya NOTE 12 ni bora mara mbili ya camera ya Galaxy A23. Selfie camera zimekuwa zikipendelewa sana hasa na wakina dada hii inawapa wepesi wakujichukua picha wenyewe pasipo kumsumbua mtu mwengine lakini ili kuweza kufurahia picha yako kwanza zingatia Pixel za kamera zisiwe chini ya Megapixel 16. Sijaongelewa kamera ya nyuma sababu zinashabihiana ni 50 kwa simu zote mbili.

Ø  CPU – Infinix NOTE 12 processor G96 / Galaxy A23 processor SD680

NOTE 12 inatumia Mediatek G96 na A23 inatumia snapdragon 680 zote ni CPU nzuri na zenye kasi isipokuwa kama wewe ni mpenzi wa games basi Infnix NOTE 12 inakufaa zaidi kufurahia games. Mediatek ni processor nzuri sana na yenye kasi ikija kwenye games kulinganisha na snapdragon.

 


Ø  upatikanaji

Infinix NOTE 12 inapatikana kwa bei ya shillingi 490,000 na kwa mujibu wa mtandao wa kijamii @infinixmobiletz katika kipindi hiki hadi tarehe 9Septemba ukinunua NOTE 12 unajiweka katika nafasi ya kujishindi DSTV decorder, laptop, Smart TV au NOTE 12 vip mpya na Samsung inapatika kwa bei ya sh. 515,000 za Kitanzania.

Tupigie kwa namba hii 0743558994 na utuambie ungependa kujua nini kuhusu teknolojia.

 usiache kuendelea kufatilia page na kurasa zote za zoom tech kwa taarifa zaidi.


#TechLazima.

 

13 Maoni

  1. Huwezi fananisha samsung na infinix ..samsung ina qualit ya hd kwenye picha no stack kwenye function cyo km infinix..

    JibuFuta
    Majibu
    1. Kiukwer inifinx ni sm nzuri sana tofauti na sm nyingine kwa hapo samsung na inifinx uwezi kutofautisha endapo zitakuwa azina majina

      Futa
  2. TATIZO KWA SANSNG HAIKAI MOTO

    JibuFuta
    Majibu
    1. Infinix ndio sim nzuri zaidi yenye maitaji mtu anataka km camera nzur kudum na chaj nk naipenda infinix

      Futa
    2. Tatizo ya Samsung ni chaji unakula sana , naomba muboleshe beteli yake.

      Futa
  3. Kazi nzuli na mm nitakuwa mmoja wapo kutumia infinix

    JibuFuta
  4. Naitumia na sitohama iphinix ni kiboko

    JibuFuta
  5. Me binafsi natumia infinix hot 7 na ni nzuri

    JibuFuta
  6. I love u Infinix mko poaa saaaanaaaa

    JibuFuta
  7. Infinx Iko poa kuliko

    JibuFuta
  8. عمل جميل جدا

    JibuFuta
  9. Infinix kiboko wala sihami huko

    JibuFuta
  10. Natumia Infinix hot 10 lite naikibali sana na sihami!!!!!!!!!!

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi