Kama haukuwa unafahamu Infinix ZERO ULTRA 5G imeshatua katika soko la simu nchini Tanzania hivyo basi leo tutaiangaza kiundani kwa kuidadavua kila feature ya simu hii.
FAST CHAJI WAT 180
Kwanza kabisa simu hii hukupa utendaji mzuri kwa bei nafuu, kimuonekano na kiufanisi ni bidhaa nzuri kwa vijana wa kisasa. Ukweli usiopingika inauwezo mkubwa wa kupitisha chaji kwa dakika 12 mbili tu kwa simu iliyokwisha kabisa kufikia asilimia 100, kwa mujibu wa tovuti mbalimbali hii ndio simu ya kwanza duniani kuja na fast chaji ya wat 180 na kuthibitishie uhodari huu wa kuchaji kwa haraka si wa muda tu bali ni milele pale tu unaporuhusu kitufe cha FURIOUS MODE wakati wa kuchaji.
CAMERA MEGAPIXEL 200 na OIS.
Kingepengele cha kamera nacho ni
yakinifu Megapixel 200 pamoja na teknolojia ya OIS, 4k kwa 30fps hadi 60fps kwa
resolution ya 1080. Teknolojia hii ya OIS utendaji mkuu wa feature hii ni
kuimarisha picha ambayo itachukuliwa katika hali ya mtikisiko. Infinix ZERO
ULTRA ni simu aminifu kwa vijana ambao kazi zao zinategemea kamera, kamera ya
mbele na nyumba kwa pamoja zinauwezo wakupiga picha au kuchukua video kwa
wakati mmoja.
MEDIATEK DIMENSITY 920
Infinix imeweka ZERO ULTRA na
kichakata kazi cha Mediatek Dimensity 920 6nm 5G kwa utendakazi ulioboreshwa,
muunganisho wa kuwezesha WI-FI 6, 5G SIM na Erdal Engine 3.0 kwa matumizi ya
kuaminika na yenye nguvu kwenye mitandao na uchezeshaji wa games ikiunganishwa na
Rom ya GB 256 kwa matumizi ya uhifadhiji kumbukumbu na Ram ya GB 13 ikiiwezesha
ufunguaji wa application nyingi kwa wakati mmoja.
3D AMOLED DISPLAY 120HZ
Umbo la 3D lenye muonekano wa
kuvutia kama ilivyo kwa simu za Samsung S series, kioo cha inch 6.8 FHD+ AMOLED
na refresh rate 120Hz resolution 2400*1080 huonyesha muonekano salama na
wakuvutia katika uangalizi wa picha, video na application nyingine zote kwa
ujumla ni simu imarika kabisa kwa kijana mwenye kuitumia simu kama kitendea
kazi katika shuhuli za masomo na kiofisi.
NDANI YA BOX
utapata nyaraka Fulani, Klabu ya
X-Gold ya dola moja, kebo ya aina ya C ‘type c’ ya 3.5mm, pini na kichwa cha
chaji cha wat 180 pamoja na simu yenyewe.
WARRANTY
ZERO ULTRA imekuja na ukadiriaji wa
ufasaha wa TUV SUD wa miezi 36, kumaanisha kuwa watumiaji wana uhakika wa miezi
36 ya ubora kamilifu.
kwa maelezo zaidi pia unaweza kupiga number +255 712 602 970 kufahamu kuhusu Infinix zero ultra

Bei
JibuFutaNi 1500000
FutaMkuu inapatikana kwa bei ya kuanzia 1.3M mpaka 1.5M
FutaSimu nzuri sana hii, ni shiling ngapi?
JibuFutaMkuu inapatikana kwa bei ya kuanzia 1.3M mpaka 1.5M
FutaNamini ikopoa na itanivutia sana
JibuFutaHakika mkuu, Nzuri sana
FutaShingap hiyo simu mbona kama n fire
JibuFutaShingapi hiyo sim
FutaMkuu inapatikana kwa bei ya kuanzia 1.3M mpaka 1.5M
FutaNataka nihame kwenye Note 11 Pro ebu taja bei ikoje aisee
JibuFutaMkuu inapatikana kwa bei ya kuanzia 1.3M mpaka 1.5M
FutaShingap
JibuFutaMkuu inapatikana kwa bei ya kuanzia 1.3M mpaka 1.5M
FutaNgapi
JibuFutaMkuu inapatikana kwa bei ya kuanzia 1.3M mpaka 1.5M
FutaKiukweli nimefurahishwa Sana na simu hyo hususani chaji yake 🤗🤗
JibuFutaSimu nzur xana lkn bei mbili tofauti hii imekaaje ufafanuzi tafadhari.
JibuFutaBei mue mnazielekeza kwaulefu tukajua Zaid kuliko ivyo mnavyo fanya
FutaChapisha Maoni